KALINJUMA DEZIDERY 2010-04-06330
NI KWA JINSI GANI TAFSIRI HUSAIDIA KUKUZA NA KUSAMBAZA FASIHI?
Makala hii ilikuwa moja ya kazi za utafiti wa kujisomea. Kazi hii iliandaliwa na kwa silishwa kwa wanafunzi kama kazi ya tendi za Kiswahili.
Utangulizi.
Makala hii inaelezea kuhusu tafsiri na nafasi yake katika kukuza na kusambaza fasihi, katika makala hii nitaanza kwa kueleza maana ya fasihi linganishi maana ya tafsiri kama ilivyofafanuliwa na wataalamu mbalimbali. Baada ya tafsili nitachambua tafsiri katika fasihi linganishi ya Kiswahili mkazo ukiwa zaidi katka mchango wake kama nyenzo muhimu katika kukuza fasihi. Pia makala hii itaonyesha utanzu ulioingiza kazi za fasihi za kigeni kwa njia ya tafsiri, utanzu unaokabiliwa na changamoto nyingi wakati wa kutafsiri na namna ya kukabiliana na changamoto hizo. Sehemu inayofuata ya makala hii itaonyesha kwa kina utanzu mmoja kati ya zilizopo kwenye jedwali kama kielelezo cha kueleza ubovu au ubora wa kazi za fasihi na kisha utafuata uchambuzi wa kazi mojawapo ya fasihi msisitizo ukiwa hasa kwenye mchango wa tafsiri katika fasihi linganishi ya Kiswahili pamoja na changamoto zitokanazo na mchakato wa tafsiri katika kufasiri matini za kifasihi. Nikianza na maana ya fasihi linganishi na maana ya tafsiri kama zilivyoelezwa na wataalamu mbalimbali.
Wamitila (2003) anaeleza kuwa fasihi linganishi inahusu uchambuzi wa maandishi ya wakati mmoja na aina moja na katika lugha mbalimbali kwa nia ya kumiliki sifa zinazoyahusisha kama athari, vyanzo, sifa zinazofanana na tofauti za kiutamaduni. Anaendelea kueleza kuwa inawezekana kufanya hivi kwa nia ya kuangalia matapo mbalimbali, maendeleo au hata nadharia za kiuhakiki. Fasihi ya namna hii iliweka misingi na juhudi za wanaisimu kuanza kuilinganisha lugha mbalimbali katika karne ya kumi na tisa. Hivyo tunaweza kusema kuwa faasihi linganishi inajikita zaidi kutumia mbinu za kiulinganishi baina ya kazi mbili za kifasihi ili kujua sifa fulani fulani kama vile kufanana kwa kazi hizo, tafauti za kiutamaduni katika kazi hizo, kujua ulinganishi katika lugha yaani sarufi ya lugha katika kazi hizo za kifasihi.
Dhana ya tafsiri imejadiliwa na wataalamu wengi kama Mwansoko na wenzake (2006) Pia wakimnukuu Catford (1965), Naye Newmark (1982) Nida na Taber (1969) waanaekea kufanana katika fasili zao kwani Newmark na Mwansoko wanasema kuwa ni zoezi la kuhawilisha ujumbe kutoka matini chanzi kwenda matini lengwa, wakati Catford anasema ni kuzalisha upya ujumbe
\
ulio katika matini chanzi katka matini lengwa na Nida na Taba wanasema ukuwa ni kuzalisha upya ujumbe wa lugha chanzi kwa kutmia visawe vya asili vya lugha lengwa vinavyo karibiana na lugha chanzi kimuundo na kimaana. Hivyo tunaweza kuona kuwa wataalamu hawa walicholenga ni kufikisha ujumbe wa matini cha nzi katika matini lengwa. Baada ya kuona fasili ufuatao ni umuhimu wa tafsiri katka fasihi.
Tafsiri ni nyenzo muhimu katika kukuza na kusambaza fasihi. Tafsiri ndilo daraja linalo unganisha jamii za watu wanaotumia lugha zinazotofautiana. Katika kufanya hivi kuna uibukaji wa misamiati mipya ambayo hapo awali haikuwepo katika lugha Fulani G. Ruhumbika katika Makala za semina ya kimataifa ya waandishi wa Kiswahili (ii) anaeleza kuwa maneno ya kigeni katika lugha nyingine ni ya msingi sana na tunaendelea kuyahitaji sana. Maneno haya yanakubalika na yanatumika mpaka sasa. Maneno katika lugha yanaweza kuingizwa ka kutoholewa, kukopwa, kuhawilishwa nkadhalika.
Fasihi ya Kiswahili imeanza kuchapishwa nje ya chi na bara la afrika. Mwansoko na wenzake (2006) wanasema ‘shughuli za wazalendo zimejalizwa na mashirika ya ufasiri na uchapishaji ya nchi za nje ambayo yamefanya kazi kubwa ya kupanua hazina ya vitabu vya Kiswahili. Baadhi ya mashirika hayo ni shirika la uchapishaji lugha za kigeni, Beijing china, shirika la uchapishaji la maendeleo na shirika la uchapishaji la Ruduga yote ya Moscow, Russia, Longmans nk. Miongoni mwa tafsiri za Kiswahili za mashirika haya ni pamoja na shajara ya mwenda wazimu na hadithi teule za Lu Kun. Kutokana na maendeleo tafsiri fasihi ya Kiswahili imesambaa na kuwafikia watu wa mataifa mbalimbali.
Waandishi wengi wamejifunza mbinu za uandishi kutoka mataifa mengine. Mfano mtindo wa uandishi, ujenzi wa wahusika na ubunifu wa mandhari na mbinu nyingine za kisanaa. Hii imeifanya fasihi ya Kiswahili kukua na kuweza kufanyiwa ulinganisho na fasihi nyingine za kilimweengu mfano tamthiliya ya Amezidi ya Said A. Mohammed. Waandishi wengine kama Kezilahabi, Pamoja na wamitila. Waandishi hawa waliandika kazi zao sambamba na fasihi za kiulimwengu. Hivyo huenda ni kutokana na kusoma kazi nyingi za tafsiri wameweza kuibuka na
aina hii ya uandishi iliyo ikuza fasihi ya Kiswahili hadi kufikia ngazi moja na fasihi za kilimwengu.
MAPITIO YA KAZI ZA FASIHI ZILIZOTAFSIRIWA
|
JINA LA KAZI
|
UTANZU
|
MFASIRI
|
MWAKA
|
TAFSIRI
|
|
|
|
|
|
|
1.
|
Barua ndefu kama hii.
|
Riwaya
|
C. Maganga
|
1994
|
Kifaransa-Kiswahili
|
2.
|
Wema hawajazaliwa
|
Riwaya
|
A.Abdallah
|
1996
|
Kiingereza-Kiswahili
|
3.
|
Alfa-lela ulela namba kitabu 2.
|
Hadithi fupi
|
Hassan Adam
|
2004
|
Kijerumani-kiswahili
|
4.
|
Alfa-lela ulela kitabu 4
|
Hadithi fupi
|
Edwin W. Brenn
|
1994
|
Kiingereza-Kiswahili
|
5.
|
Robinson crusoe
|
Hadithi fupi
|
Genesis Press Kiswahili
|
2010
|
Kiingereza-Kiswahili
|
6.
|
Wimbo wa lawino
|
Ushairi
|
P. Sozigwa
|
1975
|
Kiingereza-Kiswahili
|
7.
|
Sundita
|
Tamthiliya
|
E. mbogo
|
2011
|
Kiingereza-Kiswahili
|
8.
|
Aliyeonja pepo
|
Tamthiliya
|
Martin Mkombo
|
1980
|
Kiingereza-Kiswahili
|
9.
|
Nitaolewa nikipenda
|
Tamthiliya
|
C. Mkabugi
|
2010
|
Kiingereza-Kiswahili
|
10.
|
Orodha
|
Tamthiliya
|
S. D. Kiango
|
2006
|
Kiingereza-Kiswahili
|
11.
|
Mkaguzi muungwana
|
Tamthiliya
|
A.Morrison
|
1961
|
Kiingereza-Kiswahili
|
12.
|
Mnafiki
|
Tamthiliya
|
L.Taguaba
|
1973
|
Kiingereza-Kiswahili
|
13.
|
Mfalme edpode
|
Tamthiliya
|
S.S. Mushi
|
1971
|
Kiingereza-Kiswahili
|
14
|
Masaibu ya ndugu jero
|
Tamthiliya
|
A .S. Yahya
|
1974
|
Kingereza- Kiswahili
|
15
|
Mkaguzi mkuu wa serikali
|
Tamthiliya
|
C. Mwakasaka
|
1979
|
Kingereza-kiswahili.
|
16
|
Mnafiki
|
Tamhiliya
|
L. Taguaba
|
1973
|
Kingereza-Kiswahil .
|
Kazi ya tafsiri ni nyenzo kubwa katika kueneza na kukuza fasihi kwani kutokana na kazi kutafsiriwa kutoka lugha mbalimbali huifanya lugha hiyo ikue kwa kuongeza msamiati na idadiya watumiaji. Baada ya kuona umuhimu ifuatayo ni tathimini ya kazi ya tafsiri.
KALINJUMA DEZIDERY 2010-04-06330
Katika kutathmini mapitio ya kazi za tafsiri zilizotafsiriwa kutoka lugha mbalimbali, utanzu wa tamthiliya unaonekana kutafsiriwa zaidi na kuingiza kazi za kiafasihi nyingi za kigeni kuliko tanzu nyingine. Hii ni kwa sababu;
Hutafsiriwa ili isomwe na hutafsiriwa ili iweze kuigizwa jukwaani. Kutokana na mchezo wa uigizaji kuwa kichocheo kikuu cha kuburudisha jamii, tamthiliya imepata sifa ya kutasiriwa zaidi ili
iweze kuigizawa jukwaani. Pia kutokana na muundo wake wa majibizano ambao huleta hamu an kuvuta hisia wakati wa usomaji umefanya kuwepo na wahitaji wengi wa kusoma tamthilya hivyo kikawa chanzo cha kufasiriwa zaidi. Mifano iko katika jedwali.
Lugha zilizojitokeza katika kufanikisha suala la tafsiri ya Kiswahili ni kiswahili kwani kutokana na idadi ya tafsiri nilizokusanya, tafsiri nyingi zinaonekana kutafsiriwa kutoka kiingerza kwenda Kiswahili na nyingine chache zimetoka lugha ya Kikerewe, kijerumani, na kifaransa. Hii ni kutokana na data nilizo kusanya.
Utanzu uokabiliwa na changamoto zaidi wakati wa kutafsiri ni ushairi. Newmark (1988)anasema ushairi ndiyo utanzu wa fasihi uliomgumu zaidi kutafsiri. Utanzu wa ushairi huwa mgumu kutokana na kuandikwa kisanii zaidi ili kulidhisha na kufurahisha nafsi ya mwandishi. Ushairi huzingatia zaidi vipengele vya fani. Jambo la kwanza la maana katika kutafsiri ushairi ni neno likifuatiwa na msitari. Tofauti na zilivyo tanzu nyingine za fasihi. Licha ya kubeba maana za kawaida neno katika ushairi aghlabu huwakilisha sauti na milio mbalimbali ambayo mfasiri lazima aioneshe pia katika matini lengwa ili ujumbe uliokusudiwa ufike.
Katika kutafsiri ushairi lazima kuzingatia vipengele vyote vya fani kama sitiali, tamathali za semi, ishara, tashibiha na vingine. Hivyo ni lazima kila neno na mstari katika ushairi vizingatiwe kwa uzito uleule kama ulio katika matini chanzi. Mfano kama sitiari au ishara, sauti zina visawe katika lugha chanzi basi vitafutiwe visawe katika lugha lengwa ili kutimiza uhalisia wa lugha chanzi.
Hivyo ni vigumu kufasiri ushairi kutokana na uteuzi wa lugha katika matini chanzi. Na ni vigumu sana kwa shairi lililo tafsiriwa kulingana na shairi chasili katika uzito wake. Ili kuepuka changamoto hizo lazima mfasiri ajue utamaduni wa lugha chanzi na lugha lengwa ili kuweza kufasiri kulingana na utamaduni wa jamii lengwa. Pia mfasiri anaweza kufasiri kulingana na jinsi shairi linavyomwingia au linavyomchoma na kumwathili yeye mwenyewe yaani mfasiri ajichukulie yeye ndiye mlengwa wa tafsiri anayoifanya.
Katika kubainisha ubora au udhaifu wa tafsiri nimeteua tamthiliya ya “Black hermit” kilichoandikwa na Ngugi wa Thiong’o (1968) na kutafsiriwa kama “Mtawa mweusi” na EAEP ltd (2008). “Black Hermit” Katka kuchambua kigezo hiki cha ubora na ubovu wa tafsiri nimegundua kuwa tafsiri ya “Mtawa mweusi” ni tafsiri bora kiasi kwani ameweza kuzingatia vpipengele vilivyo katika matini chanzi mfano ujumbe, miundo ya maneno, alamaza uandishi na nyingine. Lakini kuna makosa ambayo mfasiri huyafanya wakati wa tafsiri ambayo kiuhakika yanaweza kuiwekwa tamthiliya hii katika ubovu mafano: uongezaji wa maana, udondoshaji wa baadhi ya vipengele, kuacha baadhi ya maneno, uteuzi mbaya wa msamiati ambao hubadili lengo la matini chanzi, kubadili muundo wa matini chanzi na upotoshaji ambao hupoteza maana ya matini chanzi.
Kutokana na uchambuzi wa tamthiliya ya “Mtawa Mweusi” nimegundua kuwa tafsiri ina mchango mkubwa katika fasihi linganishi ya Kiswahili. Kwa kulejelea tafsiri ya Mtawa Mweusi tunaweza kugundua utamaduni wa jamii fulani mfano tunaona utamaduni wa jamii ya Marua ambayo imejaa mambo mengi ya kulinganisha na jamii nyingine. Mfano kurithi wajane, kukatazwa kuoa nje ya utamaduni nk.
Mfano; mara baada ya hapo baba yangu akawa mgonjwa alikuwa na mshutuko baada ya kifo cha kaka yangu! Aliniita kitandani kwake akaaniambia “Remi unafahamu desturi yetu mke wa kaka yako sasa ni mkeo”
Mfano huu unatudhirishia uwepo wa utamaduni wa kulithishana wamawake katika jamii ya Marua. Ikilinganishwa na jamii ya leo hii katika afrika bado utamaduni huo upo katika baadhi ya jamii.
Tafsiri pia inatujuvya kuhusu historia ya jamii fulani ambayo inaweza kulinganishwa na jamii nyingine katika vipindi mbalimbali vya mapitio katika kuelekea maendeleo. Jamii ya marua imepitia vipengele tofauti tofauti vya maendeleo vivyojaa misuko suko ya kukataliwa kusikilizwa maoni yao, kunyanyaswa, kusalitiwa na kuvymwa haki yao. Mfano;
Lakini kwanini kumnyang’anya mfanya kazi chombao hicho kimoja atumiacho? Chama chochote cha wafanyakazi bila kugoma ni mfano wa samba asiye na makucha wala meno
Umuhimu mwingine wa tafsiri katika fasihi linganishi ni pamoja na kutujuvya kuhusu itikadi ya jamii Fulani. Katika yafsiri hii nimeweza kugundua itikadi za aina mbili, itikadi ya kaifrika juu ya wazungu na itikadi ya wazungu juu ya waafrika. Hii inawakilishwa na jamii ya marua ambayo haiwezi kuoa nje na kabila lake hasa mzungu. Hii wanaihusisha na athari waliyopata wakati wa ukoloni. Mfano Remi anakataa kumuoa Jane kwa sababu ya tofauti ya kabila na itikadi. Mfano.
Remi: “Wewe ni tofauti na mimi, na sisi, na kabila. Huwezi kufahamu yale ninayo fahamu. Oh nafahamu baba yako hakuwa mlowezi, alikuwa mwalimu mmoja wa wawatu wema…”
“Tunawezaje kuwa sawa? Wito wa kabila unawezaje kuwa wito wako”?.
Maelezo haya kiujumla yanaonesha kuwa kabila la marua hawakuwa tiyari kuwaoa watu walio nje ya kabila lao mfano wazungu. Kuhusu itikadi ya wazungu, wao hawaoni haja ya kutengana kutokana kwasababu ya rangi za ngozi zao au kabila bali wao wanasisitiza uelewano tu akti ya mtu na mtu.
Mfano: Jane
“Maana watu wote ni wamoja kila mahali. Hoja siyo utaifa, imani wala mila bali kama watu wanaweza kuelewana wao kwa wao.”
Kuligana na maelezo haya, yakilinganishwa na hali ya kawaida katika kabila mabalimbali hayatofautiani kwani ni jamii nyingi za kiafrika itikadi zake zinatofautiana na za wazungu.
Pamoja na tafsiri inayofanyika, kuna changamoto zinazotokana na mchakato wa tafsiri. Chanagamoto hizo zinatokana na hoja moja kuu sana ambayo I ukosefu wa ujuzi juu ya lugha inayotumika katika tafsiri lengwa. Mfano wafasiri wa lugha ya Kiswahili hukosa umahili walugha ya lugha lengwa. Tatizo hili ndilo chanzao cha kiila changamoto katika tafsiri. Changamoto zitokanazo na kukosa ujuzi wa lugha ni pamoja na; uteuzi mbaya wa msamiati, kushindwa vipengele vya kisarufi, kuongeza maana isiyohitajika, kupunguza vipengele vya msingi katka matini chanzi, kuacha bila kufasiri baadhi ya vipele.
Changamoto nyingine ni pamoja na tofauti kitamaduni, tofauti za kimazingira, tatizo la kiisimu, itikadi tofauti,
Kwa kuitimisha naweza kusema kuwa tafsiri ni kipengele muhimu katka kujua na kujifunza mambo mengi kutoka katika jamii tofauti.
Marejeo
East African Educational Publishers Ltd (2008) Mtawa Mweusi. Kenya: Sitima Printers
Stationers Ltd
Mwansoko, H.J.M. na wenzake (2006) Kitangulizi cha Tafsiri: Nadharia nMbinu.
Dar es Salaam: TUKI.
Newmark, P. (1982) Approaches to Translation. Oxford: Pergamon.
Newmark, P. (1988) A Textbook of Translaton. London: Prentice Hall.
Ngugi wa Thing’o (1968) Black Hermit. Kampala-Uganda: East African Educational
Publishers Stationers Ltd
Nida, A. E. na Charles, R. T. (1969) The Theory and Practice of Translation. Netherlands:
EJ. Brill.
Ruhumbika, G. (1978) “Tafsiri za Kigeni katika Ukuzaji wa Fasihi ya Kiswahili” Makala
kwenye Semina za Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili Dar es Salaam.
Mohammed S.A. (2003) Amezidi. Nairobi : East African Educational Publishers.
Wamitila, K. W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Publication
TENDI ZA KISWAHILI.
CHUO
KIKUU CHA DAR ES SALAAM
TAASISI
YA TAALUMA ZA KISWAHILI
TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA
UTENDI: SHUJAA LIYONGO
NA EMANUEL (YESU) KATIKA BIBLIA
|
YALIYOMO
SEHEMU YAKWANZAUtanguliziSEHEMU YA PILIHISTORI YA SHUJAA FUMO LIYONGO NA EMANUEL1.1 Historia ya Shujaa Fumo Liyongo1.2 Historia ya Shujaa EmanuelSEHEMU YA TATUTaswira ya Kifo cha shujaa Liyongo na Emanuel katika BibliaSEHEMU YA NNEA. Kufanana na kutofautiana kwa shujaa Liyongo na Emanuel1.Kufanana2.Kutofautiana KwaoB. HitimishoC. MAREJEO
SEHEMU YAKWANZA
TENDI NI NINI?
Tenzi za Kiswahili zimepata mjadala mkubwa hasa katika vipengele anuai ambavyo kwa hakika ndivyo vinazibainisha tenzi za Kiswahili na hata kuzitofautisha na tenzi nyingine zisizo za Kiswahili. Miongoni mwa mambo ambayo yamepata mjadala ni upatikanaji wa historia katika tenzi za Kiswahili. Mjadala huu umekitwa katika maswali mbalimbali kama vile, tenzi za Kiswahili zinahusu nini? Kuna uwezekano wa kupata historia katika tenzi za Kiswahili? Historia zinazopatikana katika tenzi za Kiswahili zina ukweli na uhalisia wowote? Historia katika tenzi za Kiswahili inatokana na ngano au visasili? Ukweli huo ni wa kisanaa au kijamii? Na ni kwa namna gani watunzi wa tenzi wanapata historia za Waswahili? Makala haya yamelenga kujadili upatikanaji wa historia katika tenzi za Kiswahili na ukweli halisi wa kihistoria katika jamii za Waswahili.
1.0 UTANGULIZI
TENZI ZA KISWAHILI
Dhana ya tenzi imetazamwa kwa mitazamo tofauti ambayo wakati mwingine hutofautiana. Ufasili wa tenzi umekuwa ukielezwa kwa kuangalia sifa. Katika makala haya istilahi itakayotumika ni tenzi ambayo itakuwa na maana sawa na tendi hivyo istilahi zote zinatumika sawa. Wataalamu mbalimbali wamejaribu kufasili dhana ya tenzi / tendi kama ifuatavyo.
Casco (2007) anaeleza kuwa utenzi umetokana na kitenzi tenda ambacho kina maanisha kufanya tendo. Anabainisha kuwa utenzi huwa na mistari minne yenye silabi nane kwa kila kipande, mistari huwa na muungano wa matukio, unaweza kuhusu falsafa au masuala ya kidini, unaweza kutoa simulio ya kweli au ya kubuni na huwa na utangulizi, kiini na hitimisho. Mtaalamu huyu anaeleza kuwa kuna ugumu katika kutafuta kisawe mwafaka cha utenzi katika lugha mbalimbali. Baadhi wanasema wimbo, ushairi na ushairi mrefu.
Kutokana na fasili ya Casco tunapata wazo kuwa utenzi huwa na matendo katika utendaji wake. Matendo hayo hujidhihirisha unapokuwa katika masimulizi, kwa maana hiyo utenzi ulio katika maandishi hupoteza baadhi ya vionjo vya kiutendaji.
Wamitila (2003) amejadili utendi kama shairi refu la kisimulizi linalozungumzia kwa mapana na mtindo wa hali ya juu matendo ya mashujaa au shujaa mmoja. Anasema kuwa utendi huwa na sifa nyingi na huweza kuleta pamoja hadithi ya shujaa, magari, visasili, historia, pamoja na ndoto za taifa fulani.
Fasili hii inatupa utata inapoeleza utendi kama shairi refu la kisimulizi. Utata unajitokeza katika kupima urefu wa ushairi ulio katika masimulizi. Tutatumia kipimo gani kupima urefu huo? Na mpaka wa ushairi mrefu na mfupi unaanzia wapi na kuishia wapi. Fasili hiyo inahitaji maelezo zaidi ya kipimo kipi kinafaa kutumika.
Mulokozi (1996) anaeleza utendi ni ushairi wa matendo. Ni utungo mrefu wenye kusimulia matukio ya kishujaa yenye uzito wa kijamii au kitaifa. Matukio hayo yanaweza kuwa ya kihistoria na visakale.
Ufafanuzi huu wa Mulokozi umepiga hatua mbele kwa kueleza utendi kama ushairi wa matendo. Utendi hufungamana na matendo wakati wa utendaji wake. Matendo hayo huathirika utendi unapokuwa katika maandishi.
Kutokana na fasili za wataalamu hawa tunaweza kusema kuwa utendi ni ushairi unaosimulia tukio fulani kwa matendo. Usimuliaji wa tukio huambatana na matendo ambayo hufanywa na msimuliaji. Utendi unaweza kuhusu tukio lolote la kijamii ambalo laweza kuwa la kishujaa au lisiwe la kishujaa.
Makala hii imekusudia kufafanua taswira ya kifo cha shujaa katika utendi kwa kurejelea kifo cha shujaa Liyongo kama alivyoelezwa katika kitabu cha Tenzi Tatu za Kale kilichohaririwa na Mulokozi mwaka (1999) na shujaa Emanuel (Yesu Kristo) kama anavyoelezwa katika Biblia takatifu.Kabla ya kujikita katika ufafanuzi huo ni muhimu kufahamu dhana ya kifo, taswira, shujaa na utendi. Kwa kuanza na dhana ya utendi, Mulokozi (1996) anaeleza kuwa, utendi ni hadithi ya kishairi kuhusu mashujaa wa kihistoria na wa kubuni, wa jamii au taifa. Anaendelea kueleza kuwa baadhi ya tendi zina sifa za kiriwaya, ila tu badala ya kuwa katika umbo la nathari zina umbo la kishairi.Vile vile Mulokozi (1999) anarekebisha kidogo fasili yake na kueleza kuwa utendi ni utungo mrefu wa kishairi wenye kusimulia hadithi ya ushujaa na mashujaa. Ukizichunguza fasili hizi utagundua kuwa tendi zina sifa ya kishairi, zinatokana na masimulizi (zilizo nyingi), zinahusu mashujaa ambao wanaweza kuwa wa kihistoria au wa kubuni. Pamoja na sifa hizo tendi pia huhusu masuala mengine ya kijamii kama vile kutoa mawaidha kwa jamii, hivyo si lazima utendi umhusu shujaa peke yake.Dhana ya kifo inaweza kufasiliwa kuwa ni kitendo cha kutolewa uhai au kupatwa na mauti kama ambavyo Mohamed (2002) ameeleza kuwa kisawe cha kifo ni mauti au ufu. Vile vile Wamitila (2003) amefafanua dhana ya taswira kuwa hutumiwa kuelezea neno, kirai au maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika akili ya msomaji. Anaendelea kueleza kuwa, taswira zinaweza kuwa za kimaelezo ... (yaani maelezo fulani yaliunda picha) au za ki-ishara (zinazounda picha ambayo inaashiria jambo fulani au imeficha ujumbe mwingine).Kwa mujibu wa Wamitila (2003) neno shujaa, hutumika kuelezea mhusika mkuu katika kazi ya kifasihi ambaye anaweza kuwa wa kike au wa kiume. Kimsingi neno hili haliashirii wema tu.Mulokozi (1996) kwa upande mwingine ameeleza kuwa, mashujaa wa utendi wa Kiswahili ni wa aina tatu (3) ambazo ni mashujaa wa kijadi wa Kiafrika, kwa mfano Fumo Liyongo katika Utendi wa Fumo Liyongo (Mohamed Kijumwa K 1913) na Abushiri bin Salim katika Utendi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima (Hemed Abdallah K, 1895), mashujaa wa kidini, hasa mtume Muhamadi na masahaba wake (k.m. utendi wa Ras ‘lghuli) na mashujaa wa kubuni kwa mfano Tajiri katika Utendi wa Masahibu.Mulokozi anaendelea kueleza kuwa, kati ya aina hizo tatu za mashujaa, riwaya ya Kiswahili imetumia mbili tu. Wahusika wa kijadi wa Kiafrika na wahusika wa kubuni. Wahusika wa kidini hawajatumiwa kikamilifu (uk. 42) Kutokana na ufafanuzi huu ni dhahiri kuwa, mashujaa wa kidini bado hawajaelezwa ipasavyo na ndio sababu makala hii imejikita katika kuelezea angalau kwa sehemu kuhusu shujaa Emanuel katika Biblia akihusishwa na shujaa wa kihistoria na wa kijadi Fumo Liyongo katika Utendi wa Fumo Liyongo.Baada ya kufahamu utangulizi huu, sehemu inayofuata itahusu historia ya mashujaa waliokwisha tajwa hapo juu.
SEHEMU YA PILI
HISTORIA YA SHUJAA FUMO LIYONGO NA EMANUEL
1.1 Historia ya Shujaa Fumo Liyongo
Fumo Liyongo ni shujaa kama alivyoelezwa na Muhamadi Kijunwa mwaka 1913 katika Utendi wa Fumo Liyongo. Mwandishi amesimulia habari za shujaa huyu kwa njia ya maandishi katika umbo la kishairi. Japo kuna utata kuhusu tarehe aliyozaliwa Liyongo lakini tarehe inayoelekea kukubaliwa zaidi ni ile ya karne ya 13 – 14 kwa kuwa kitabu cha Terehe ya Pate (Freeman-Grenville 19962: 241 – 299) kinamtaja mtawala wa eneo la Ozi aitwaye Fumo Liyongo aliyeishi wakati wa utawala wa Fumomari (Fumo Omari), mtawala wa ki-Nabhany wa dola ya Pate. Fumomari alitawala miaka ya 740 – 795 Hijriya (Miaka ya Kiislamu), sawa na 1340 – 1393 M. Liyongo huyo alipigana na Fumomari (Mulokozi 1999).Mwandishi huyu anaendelea kutujuza kuwa vyanzo vinaonesha kuwa Liyongo aliishi Pwani ya Kaskazini mwa Kenya kwenye maeneo ya Pate na Ozi kwenye karne ya 14 au kabla. Mama yake aliitwa Samoa mwana. Liyongo alikuwa kiongozi katika jamii yake, japo hakuna uhakika kama alikuwa mfalme. Alikuwa shujaa, manju wa ngoma na malenga, na mwindaji hodari. Kwa upande wa dini, hakuna uhakika kama alikuwa ana Mkristo au Mwislamu japo nyimbo zake zinaonesha kuwa huenda alikuwa mfuasi wa dini ya Jadi ya Waswahili. Liyongo alikuwa akiwinda na kufanya biashara sehemu za bara karibu na Pate, aliweka makazi yake Ozi, na alifia na kuzikwa Kipini, mahali paitwapo Ungwana wa Mashaha (Mulokozi na Sengo 1995:52-53). Ubeti wa 230 unaeleza kwa muhtasari maisha ya shujaa Fumo Liyongo1.2 Historia ya Shujaa Emanuel
Emanuel ni shujaa wa kidini ambaye anaelezwa katika maandiko matakatifu yaani Biblia. Kuzaliwa kwa shujaa huyu kulitabiriwa na nabii Isaya (Isaya 9:6) sura ya 9 kifungu / mstari wa 6.Tangu utabiri wa Isaya hadi kuzaliwa kwake inakadiriwa kuwa ni miaka 400 k.k. Utabiri wa nabii Isaya ulitimia katika kitabu cha Mathayo 2:1 ambapo inaeleza kuwa shujaa alizaliwa Bethlehemu ya Uyahudi zamani za Mfalme Herode. Kama ilivyo desturi ya mashujaa wengi wa kidini , baada tu ya kuzaliwa alikutana na vikwazo vya kutaka kuuawa na Mfalme Herode ambaye alihofia kunyang’anywa madaraka, shujaa huyu atakapokuwa mkubwa (Math 2:13). Malaika wa Bwana alimtokea Yusufu (Baba wa Emanuel) katika ndoto kumweleza kuwa amchukue mtoto Emanuel na mama yake (Mariam) kisha wakimbilie Misri. Ndivyo ilivyo hata kwa mashujaa wengine, misukosuko inapozidi kukimbilia uhamishoni. Baada ya Mfalme Herode kufa shujaa Emanuel alirudishwa na wazazi wake Galilaya katika mji wa Nazareti.Shujaa Emanuel alibatizwa na Yohana katika mto Yordani. Baada ya kubatizwa Roho wa Mungu alishuka juu yake kisha sauti ilisikika kutoka mbinguni ikisema “Huyu ni mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye” (Math 3:13 – 17). Shujaa huyu alibatizwa akiwa mtu mzima yapata miaka 27. Baada ya kubatizwa alipelekwa na Roho Mtakatifu nyikani ili ajaribiwe na ibilisi, alifunga siku arobaini, mchana na usiku, kisha alishinda majaribu yote ya Ibilisi (Shetani) (Math. 4:1 – 11).Baada ya shujaa Emanuel kutoka nyika ni alichagua wanafunzi (wafuasi) kumi na mbili (12) ambao alikuwa anafanya nao kazi, na ndipo alipoanza huduma ya kuihubiri habari njema ya Ufalme wa Mungu na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna kwa watu (Math 4:17 – 25) akiwa na miaka 27. Baadhi ya wanafunzi, wake ni Simoni Petro, Andrea, Yohana. n.k. Habari za shujaa huyu ilienea kutoka Galilaya, Dehapoli, Yerusalemu, Uyahudi na ng’ambo ya Yordani. Shujaa Emanuel alifanya huduma kwa muda wa miaka mitatu kisha akafa. Wakati wa huduma ya kuwakomboa watu na dhambi zao, wapo waliomkubali na kumfuata na wengine walimchukia na kumshutumu kuwa alikufuru kwa kujiita mwana wa Mungu. Wale waliomchukia ndio waliofanya njama za kumuua. Hatimaye walimtumia mmoja wa wanafunzi wake aliyeitwa Yuda kwa kumpa vipande 30 (thelathini) vya fedha ili amsaliti kisha wamkamate. Yuda aliwaambia, nitakayembusu ndiye, na hapo ndipo Wayahudi walipomkamata shujaa huyu na kumsulubisha hadi kifo chake (Marko 14:10-72 na 15:1-37).SEHEMU YA TATU
Taswira ya Kifo cha shujaa Liyongo na Emanuel katika Biblia
1. Taswira ya Kifo cha shujaa LiyongoLiyongo ni shujaa aliyependwa na watu kwa kuwa aliwapigania na kuwasaidia, mfano aliwasaidia Waggala kupata mbegu bora (ub 40 – 41), aliishi porini na Watwa na kushirikiana nao vizuri, ushirikiano uliomsaidia kumnusuru na njama za mfalme za kutaka kumuua.Kutokana na uhusiano mzuri aliokuwa nao na jamii yake Mfalme anamwonea wivu na anaogopa kuwa anaweza kumpokonya madaraka (ufalme). Anafanya njama za kumuua. Njama hizo hazifanikiwi na inabidi mfalme amtumie mwanawe Liyongo ili amsaliti baba yake kwa kuahidiwa kuozwa binti mfalme, kupewa uwaziri na mali nyingi. Mtoto wa Liyongo anamuuliza babaye siri ya nguvu zake, anapoambiwa kuwa ni kuchomwa sindano ya shaba kitovuni, anakubali kumchoma baba yake hatimaye Liyongo anakufa, kisha mwanawe naye anakufa kutokana na uovu wake.Baada ya shujaa Liyongo kufa watu walisikitika, waliomboleza na wengine walionekana kukata tamaa kwa kuwa shujaa huyu alikuwa ni mtetezi wa watu katika jamii. Beti za 224 – 226 zinaeleza vizuri jinsi watu walivyomwombolezea shujaa wao.Taswira ya kifo cha shujaa Liyongo inaweza kujitokeza kwa namna tatu (3). Kwanza kifo cha shujaa Liyongo kwa mfalme ni mafanikio kwa kuwa ana uhakika wa kuendelea kutawala maana alikuwa na hofu kuwa Fumo Liyongo atamnyang’anya ufalme kwa vile alivyokuwa na mshikamano na watu. Pili, kifo cha Liyongo kwa mwanawe ni adhabu kwani baada ya shujaa huyu kufa mwanawe naye alikufa kutokana na maradhi yasiyopona (ubeti 223) pamoja na kuchukiwa na jamii yote kwa ujumla. (beti za 217 – 222). Tatu kifo cha Liyongo kwa jamii yake ni sawa na kupoteza kitu chenye thamani kwa vile Liyongo alikuwa na mshikamano na jamii yake. Baada ya kifo chake watu wanaomboleza na wanaonekana kukosa matumaini, haya yanayojitokeza katika (beti za 224 – 227).
Kwa upande wa fasihi, kifo cha shujaa Liyongo kimejengwa katika dhana ya usaliti unaosababishwa na tamaa ya madaraka (Ufalme) na tamaa ya mali (Mtoto wa Liyongo). Mfalme (sultani) wa Pate anafanya fitina (Ubeti 49) za kumuua Liyongo akiogopa kupokonywa ufalme (ub. 93). Mwanawe Liyongo naye alikubali kumsaliti baba yake kwa matarajio ya kuozwa mke (binti wa mfalme), kupewa mali na uwaziri pia. Dhana ya usaliti imejitokeza sana katika kazi za kifasihi na inaonekana kuwa ni silaha ya kumwangusha shujaa mfano Lwanda Magere katika kitabu cha Lwanda Magere, Samsoni na Yesu katika Biblia. Kwa upande mwingine dhana hii ina sura mbili yaani faida (anayenufaika baada ya usaliti) na hasara (anayeathirika baada ya usaliti).Kifo cha shujaa pamoja na usaliti vinatupatia motifu ya dhambi na mapatilizi. Ingawa mtoto wa Liongo alimsaliti babaye ili apewe zawadi nono hakutimiziwa ahadi hizo. Alinyanyaswa na hatimaye alikufa kama alivyokufa baba yake. Hii inaashiria kuwa katika mapigano kati ya wema na uovu, siku zote wema hushinda. Kwa hiyo hata sultani hana maisha marefu. Historia imelishuhudia hili kwa kuwa muda si mrefu uatawala wa kisultani ulivamiwa na ukoloni, hata huo ukoloni nao leo hii haupo. Maisha ya milele ni maisha ya kutenda wena na haki.2. Taswira ya Kifo cha Shujaa Emanuel katika BibliaShujaa Emanuel alitabiriwa kuwa atazaliwa, atakufa na siku ya tatu atafufuka na kupaa mbinguni. Jina Emanuel lina maana ya Mungu pamoja nasi. (Math 1:22-23) maneno “Mungu pamoja nasi” yanarejesha uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu ambao ulipotea katika bustani ya Edeni baada ya Adamu na hawa kutenda dhambi. Baada ya anguko (dhambi) la Adamu na hawa, Mungu aliwaacha wanadamu kwa kuwa yeye ni mtakatifu na hashirikiani (hashikamani) na uchafu (Mwanzo 3:1 – 24).Kwa kuwa mwanadamu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu (Mwanzo 1:26 – 27), Mungu aliwahurumia na kuamua kuwaokoa tena kutoka katika utumwa wa dhambi na matendo ambayo shetani alikuwa akiwafanyia baada ya lile anguko la bustani ya Edeni. Kwa sababu hiyo aliamua kumtoa mwanawe wa pekee Yesu Kristo (Emanuel) afe msalabani ili awakomboe wanadamu. Hivyo, kila atakayemwamini shujaa Emanuel (Yesu Kristo) ataokolewa atoke katika utumwa huo wa dhambi na mateso yote ya Ibilisi na ndipo atakuwa ameunganishwa na Mungu yaani uhusiano wake na Mungu utarejeshwa tena yaani Mungu atakuwa pamoja naye.Kifo cha shujaa Emanuel, japo kilitabiriwa kwa kuwa Mungu aliamua kuwarudia tena wanadamu lakini Yuda Iskariote ndiye aliyepelekea kifo hiki kutokea. Alimsaliti Emanuel kwa Wayahudi kwa tamaa ya pesa ya vipande thelathini (30). Kama ilivyokuwa kwa shujaa Liyongo, Emanuel naye alisalitiwa na mtu wa karibu. (Mwanafunzi wake) kama Waswahili wasemavyo “Kikulacho ki nguoni mwako” (Luka 22:47). Habari za kifo cha shujaa huyu zimeelewa vizuri katika vitabu hivi: Mathayo sura ya 26-27, Marko sura ya 14 – 15, Luka sura ya 22 – 23 na Yohana sura ya 13 – 19. Yuda aliyewasaliti Yesu, baada ya kupewa vipande 30 vya fedha alimbusu Yesu, na Wayahudi, Waandishi na Mafarisayo wakamkamata na kumtesa hadi alipokufa.Taswira ya kifo cha shujaa Emanuel kinajitokeza kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo: Kwanza Wayahudi, Waandishi na Mafarisayo waliona kama wamemkomoa kwa kuwa walidai kuwa anajikweza kwa kujifanya mwana wa Mungu. Pia watawala walifurahi maana watu wengi walimfuata na kumsikiliza.Pili, kifo cha Emanuel kilipoteza matumaini ya watu waliokuwa wakimwamini, ndugu zake (k.v. wazazi) pamoja na wanafunzi wake. Watu walilia na kuomboleza pale msalabani kwa kuwa mtetezi wao ametoweka japokuwa waliahidiwa kuwa siku ya tatu atafufuka.Tatu, kifo cha Emanuel kwa Mungu kilikuwa ni kutimiza kusudi lake la kuwakomboa wanadamu, kwa kuwa alifanyika sadaka ya dhambi yaani alijitoa kafara ili wanadamu wasife tena kwa dhambi.Nne, katika muktadha wa kifasihi tunaona nguvu ya usaliti katika kumwangusha shujaa. Usaliti umeonekana ukifanya kazi au kulisababisha shujaa kuanguka. Hata katika maisha ya kawaida ya kila siku dhana hii inatenda kazi kwani tunashuhudia watu wakijiua kwa kuwa wamesalitiwa na wapenzi wao, ndugu au marafiki zao.Kwa ujumla suala la usaliti limesawiriwa vizuri katika kazi mbili za Utendi wa Fumo Liyongo na Biblia. Waandishi wamejitahidi kuonesha dhana hii kwa kuwatumia wahusika Liyongo na Emanuel. Kwa mtazamo wangu, baada ya kuwachambua mashujaa hawa naona kuwa usaliti ni kipimo kinachotumika kupima nguvu aliyonayo shujaa, na nguvu inapobainika na watu wengine ndipo anguko la shujaa hutokea. Mara nyingi anguko la shujaa husababishwa na watu wake wa karibu.
SEHEMU YA NNE
A. Kufanana na kutofautiana kwa shujaa Liyongo na Emanuel
1. Kufanana
Mashujaa hawa wanafanana katika mambo yafuatayo(i) Wote wanatumia nguvu isiyokuwa ya kawaida kutenda mambo ya ajabu (miujiza).(ii) Walikuwa na ushirikiano mzuri na jamii zao.(iii) Walipendwa na watu kiasi cha watawala kuwachukia(iv) Walifanyiwa njama za kuuawa(v) Wote walisalitiwa na watu wao wa karibu(vi) Baada ya kufa watu waliwaombolezea.(vii) Wasaliti wa mashujaa wanaahidiwa kupewa fedha, vyeo na mali nyingine baada ya kukamilisha kazi ya usaliti mfano Mfalme anaahidi kuwapa Wasanye, Wadahalo, Waboni na Watwa reale mia iwapo watamleta kichwa cha Liyongo. Pia mwanae Liyongo anaahidiwa mali, mke na cheo cha uwaziri. Pia Yuda aliahidiwa vipande thelathini vya fedha iwapo atafanikisha kukamatwa kwa shujaa Emanuel.(viii) Waliowasaliti mashujaa Liyongo na Emanuel walikufa baada ya kifo cha mashujaa hao(ix) Hawakuwa waoga, wote ni majasiri.2. Kutofautiana Kwao
Shujaa Fumo Liyongo Shujaa Emanuel (i) Fumo Liyongo alitumia nguvu ya uganga au sihiri. Hadhuriki kwa chochote isipokuwa kwa kudungwa sindano ya shaba kitovuni. (ubeti 143 – 144) (i) Alitumia nguvu za Roho Mtakatifu kutenda mambo mbalimbali k.v. kutembea juu ya maji, kuponya watu wengine (Mathayo 3:13-17, Mathayo 4: 23 – 25). (ii) Alioa mke na alikuwa na mtoto wa kiume, ana nguvu za kirijali (ii) Hakuoa wala hakuzaa (iii) Baada ya kufa hakufufuka (iii) Alifufuka na aliwatokea watu mbalimbali ili kuwadhihirishia kwamba yuko hai (Marko 16:1-14) (iv) Hakupaa kwenda mbinguni (iv) Alipaa kwenda mbinguni kuketi mkono wa kiume wa Mungu. (v) Hakufanikiwa kuikomboa jamii yake kwa kuwa alikufa (v) Japo alikufa kazi ya kuwakomboa wanadamu ilikamilika kwa kuwa kila atakayemwamini ataokolewa na kupatanisha na Mungu.B. Hitimisho
Katika kuhitimisha uchambuzi wa makala hii imebainika kuwa kila shujaa kati ya hao wawili alikuwa na wajibu fulani katika jamii yake ambao ilibidi autimize. Katika kutimiza wajibu huo shujaa lazima akutane na vikwazo ambavyo inabidi apambane na ashinde ili alete ukombozi kwa jamii yake. Katika kupambana huko, wapo watakaomuunga mkono na wengine kumpinga.Wale wanaompinga ndio hufanya njama za kumwangusha, wakifanikiwa shujaa hushindwa na wasipofanikiwa ndipo shujaa huyo hushinda na hivyo huleta mabadiliko katika jamii yake.
C. MAREJEO
Bible Societies of Tanzania and Kenya (1997). Biblia: Maandiko Matakatifu ya Mungu. The Bible Societies of Kenya and Tanzania: Nairobi na Dodoma (Mtawalia)Graf, H. (1980). The Panarama Bible Study Coarse No. 1: The Plan of the Ages (Toleo la 1 la Kijerumani – Kiswahili. Kanisa la Biblia Publishers: Dodoma.Mohamed, M.A. na Saidi, A.M (2002). Kamusi ya Visawe. East African Educational Publishers Ltd: Nairobi.Mulokozi, M.M. (1996). Fasihi ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania: Dar es Salaam.Mulokozi, M.M. (Mh.) (1999). Tenzi Tatu za Kale. TUKI: Dar es Salaam.Wamitila, K.W. (2003). Kamusi ya Fasihi, Istilahi na Nadharia. Focus Publications Ltd: Nairobi.
“UCHAMBUZI WA UTENZI WA MWANAKUPONA: MAWAIDHA KATIKA TENDI.
UTANGULIZI.Katika uchambuzi huu wa UTENZI WA MWANAKUPONA tunatarajia kuangalia vipengele kadhaa vya uchambuzi kama vile historia fupi ya mwandishi, vipengele vya fani na maudhui, na vingine vitakavyojitokeza. Katika uchambuzi huu tutaonesha moja kwa moja nafasi ya mwanamke katika kumtunza mumewe. Hii ni kazi ya uchambuzi kwa hiyo itahusisha vipele mbalimbali vya uchambuzi. Kisha tutaonesha hitimisho na marejeoHISTORIA FUPI YA MWANDISHI.
Mulokozi (1999) anatueleza kuwa Mwanakupona binti Mshamu Nabhany alizaliwa Pate mwaka 1810. Mwaka 1836 aliolewa na bwana Mohammed Is- Haq bin Mbarak. Lakini inasemekana kuwa alijulikana zaidi kwa jina la Mataka. Mwanakupona aliolewa na Bwanaa Mataka katika ndoa ya wake wengine watatu. Yasemekana kuwa Mataka alikuwa ni mtawala wa Siu na mpinzani mkubwa wa utawala wa waarabu huko Zanzibar. Mwanakupona alipata kuzaa watoto wawili na bwana Mataka ambao ni Mwana Hashimu bint Shee Mataka (1841-1933) na ndiye aliyetungiwa utenzi huu, na Mohammed bin Shee Mataka aliyezaliwa baina ya mwaka 1856 na 1858.
Tunendelea kuelezwa kuwa Shee Mataka alikuwa na watoto wengine watatu kwa wake wengine ambao ni Bakari alieyekufa vitani Pate mwaka 1855, Mohammed (mkubwa) ambaye ndiye aliyerithi utawala wa baba yake mwaka 1855 na kuendeleza upinzani uliokuwa umeanzishwa na baba yake dhidi ya utawala wa waarabu wa Zanzibar. Tunaelezwa kuwa baadaye Sayyid Majid, Sultan wa Unguja alimfanyia hila hadi alifanikiwa kumkamata na kumfungia katika Ngome ya Yesu, Mombasa ambako alifia huko mwaka 1868. Pia yasemekana kuwa baada ya kifo cha Mohammed (mkubwa) Omari alirithi utawala na kuishi hadi miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini na alishiriki katika kupinga ukoloni wa Waingereza huko Kenya.
Pia yasemekana kuwa Mohammed (mkubwa) alikuwa mshairi na alitunga tungo za ILELE SIU ILELE na RISALA WA ZINJIBARI ambazo zilihusu mapambano yake na Sultani wa Unguja, na fitina za baadhi ya raia zake wa Siu. Baadaye tunaelezwa kuwa Mwanahashimu aliolewa mara mbili na kufanikiwa kupata watoto wawili ambao waliishi hukohuko Lamu. Alikuwa ni mshairi na alitunga mashairi kadhaa. Baadaye tunaelezwa kuwa kuna maafa yalimkuta bibie Mwanakupona na yaliisibu familia yake na hata aliiamua kuondoka Siu na kuhamia Lamu ambako ndiko alikotungia utenzi wake wa mwaka 1858. Inasemekana kuwa Mwanakupona aliuandika utenzi huu akiwa ni mgonjwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo la uzazi. Alihisi kuwa asingepona, hivyo akaamua kutunga utenzi huu ili uwe ni wosia kwa binti yake ambaye angebaki bila ya uongozi wa mama.
MUHTASARI WA UTENZI.
Kijamiii, Mwanakupona ni utenzi wa kimawaidha uliotungwa na Mwanakupona Binti Msham kwa ajili ya binti yake aliyeitwa Mwanahashimu bint Mataka mwaka 1858. Utenzi huu unaonakena kuwakilisha vyema tungo za utamaduni na maonyo ya wakati huo. Mtunzi aliutunga ili kumlenga binti yake aliyeitwa Mwana Hashimu kwa lengo la kumuonya lakini pia aligusia kwa vijana wengine wa kike wapate kuusoma utenzi huu ili nao wapate maonyo hayo (Ubeti wa 94 na 95). Utenzi huu unaonekana kuibadilisha jamii ya uswahilini baada ya kuona kuwa unafaa hasa kwa malezi ya kijadi hasa kwa watoto wa kike kwa kuwafunda. Yawezekana Jambo hili ndilo linaloufanya utenzi huu uonekane kuwa msaada wa jamii hata leo hii.
Kihistoria, tunaelezwa kuwa huu ni utenzi wa kale uliokuwa unaendana na mazingira ya wakati huo. Mwandishi aliuandika kwa kuilenga jamii ya wakati ule hasa kwa kufuata mila, desturi za jadi za wakati huo kama vile heshima ya ndoa, wanawake kuwekwa utawani, kutoonesha sura zao mbele ya watu, kumtukuza mume kama Mungu wao wa pili. Pia unaonekana kuwa ulikuwa ni utenzi wa kitabaka la utawala.
Kifasihi, UTENZI WA MWANAKUPONA ni utenzi pekee wa kishairi uliotungwa na mwanamke ambao unaonekana kuleta athari kwa waandishi wengine hata kuiga mfano wake wa kutunga tungo za kimawaidha kama vile Said Karama WASIA WA BABA, Shaaban Robert katika utenzi wa HATI NA ADILI, Zainab bint Humud, HOWANI MWANA HOWANI, UTENZI WA ADAMU NA HAWA.
FANI NA MAUDHUI.
FANI.
Senkoro (2011), anaeleza kuwa fani katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaotumia msanii katika kazi yake. Mpangilio wa vitushi, (episode) UTENZI WA MWANAKUPONA ni utenzi wenye jumla ya beti 102 ambao unaanza kwa mtunzi kumwita binti yake akaribie akiwa na wino na karatasi ili asikiilize wosia. Anasema kuwa yeye alikuwa ni mgonjwa hivyo hakupata muda wa kumpa wosia binti yake. Anamwambia binti yake kuwa aanze kwa kumtukuza Mungu wake na kumwomba rehema zake. Baada ya hapo anamwambia anataka kumpa hirizi ya kinga yake na kidani cha kujipambia. Halafu anaanza kumpa maonyo aliyokuwa ameyakusudia kama vile kuheshimu mume, kumheshimu mungu, kuwa mwaminifu, kuepuka umbeya, kushika dini na mengineyo. Hayo ni kuanzia ubeti wa (1-25).
Na kuanzia (ubeti. 26-36) mtunzi anaeleza namna mwanamke anavyotakiwa kumfanyia bwana yake. Miongoni mwa mambo hayo ni kutojibizana naye, kumpa kila anachokihitaji, kumuaga vizuri kila anapoondoka, kumpokea vizuri kila anapokuja, kumpapasa na kumpepea usiku, kumkanda mwili, kumsifia kwa watu wengine, kumwandalia chakula, kumnyoa ndevu, na kumpendezesha.
Kuanzia (ubeti 37-56), mtunzi anaonesha namna mwanamke anavyopaswa kuwa yeye binafsi yaani mwanamke aliyeolewa inatakiwa awe msafi kimwili, avae vizuri na kujipamba kila siku, aombe ruhusu kwa mumewe kabla ya kutoka na akitoka asikawie kurudi na anapotembea asijifunue buibui lake na asiongee wala kunena na mtu yeyote njiani na aridhike kila anachopewa na mumewe.
Kuanzia (ubeti. 57-66) mtunzi anamwonya binti yake namna ya kuishi na watu wote kwa ujumla, yaani awe na upendo kwa watu wote bila kuangalia hadhi zao, afanye ushirikiano na wanandugu, marafiki na watu wengine pia awasaidie wanaohitaji msaada. Na atakapofanya hivyo malipo yake yatakuwa ni mbinguni.
Kuanzia (ubeti. 67-102) mtunzi anafanya dua ndefu ya kuwaombea watu wote wakiwemo watoto wake, anajiombea yeye mwenyewe, anawaombea waislamu kwa ujumla, na kisha anamalizia kwa kuwaombea wanawake wote wauosome utenzi huu ili wanufaike nao.
Hivyo tunaona kuwa japokuwa mtunzi amejitahidi kupangilia vitushi lakini inaonesha wazi kuwa amechanganya baadhi ya beti, yaani beti ambazo zilitakiwa ziwepo mwishoni amezipeleka kati ama mwanzoni mwa utenzi, na za mwanzoni kuzipeleka mwishoni ikiwa zingepaswa kuendana na beti fanani ili kukamilisha wazo. Kwa mfano beti za 92 na 93, zilipaswa kuwekwa mwanzoni maana zina mawazo ya mwanzoni kama vile maonyo kwa ujumla, ubeti 22 na 23 zingepaswa kuwekwa kati ya ubeti wa 11na 14 ili kusisitiza suala la dini, na ubeti wa 40 na 42 zingepaswa kuwekwa kati ya ubeti wa 36 na 37 ili kumwonya mtoto wa kike kuwa na tabia nzuri hasa kwa bwana yake kwa kuwa msafi na kufanya kazi.
Matumizi ya lugha, mwandishi huyu hajatumia sana lugha ya picha kama vile sitiari, tashibiha, tashihisi, methali nahau hata vitendawili na taswira japokuwa kwa kiasi fulani anaonekana kutumia lugha ya taswira kama vile hirizi, akionesha kuwa ni kinga ya kujikingia mtu aliyepatwa na matatizo ubeti ( 8-10), kidani,kama lulu au pambo (ubeti. 40) Anasema kuwa;Na kidani na kifungoSitoe katika shingoMuili siwate mengoKwa malashi na dalia
Hapa tunaona kuwa mwandishi ametumia taswira ya kidani inayomaanisha kuwa ni pambo au lulu inayovaliwa shingoni.
Misamiati, aliyoitumia sio migumu sana inaeleweka japokuwa kwa kiasi kikubwa ametumia lahaja ya Kiamu na anaonekana kuimudu vyema lugha yake, lakini kwa mtu asiye mmilisi wa lahaja hiyo anaweza kupata mkanganyiko pindi anapousoma utenzi huu.Muundo, kwa upande wa muundo mwandishi anaonekana kujitahidi kwa kiasi kikubwa kwani ametumia ushairi wa kufuata urari wa vina na mizani kwa kiasi kikubwa, na kila mshororo unaonekana kuwa na mizani 8.
Motifu, iliyojitokeza katika utenzi huu ni motifu ya msako wa peponi, yaani ile ya kumsaka Mwenyezi Mungu hasa kwa kutenda matendo mema, kutii maagizo yake pamoja na mwanamke kumheshimu mume. Mfano (Ubeti. 26-27) unasema;
26. Siku ufufuliwaoNadhari ni ya mumeoTaulizwa atakaoNdilo takalotendewa
27. Kipenda wende peponiUtakwenda dalhiniKinena wende motoniHuna budi utatiwa
Beti hizi mbili zinatudhihirishia kuwa Mwanakupona aliona kuwa safari ya kufika peponi ni kubwa kwani kinachotakiwa ni kujipanga ili tuweze kuepuka adhabu ya jehanamu. Anamwambia mwanaye kuwa ili kushinda hilo ni vyema kumpenda mumewe na kumtii maana huko mbinguni Mungu atamuuliza kama alimpenda na kumtii huku duniani (Ubeti.28).
Keti naye kwa adabuUsimtie ghadhabu
Akinena simjibu
Itahidi kunyamaa.
Ushujaa, wahusika wanaoelezwa katika utenzi huu sio mashujaa kama ilivyozoeleka katika tenzi zingine kama vile FUMO LIONGO, SUNDIATA, MAJIMAJI na zinginezo. Huu unaonekana kuwa ni utenzi wa kimawaidha ambao hauonyeshi ushujaa au unguli kwa sababu unatoa mawaidha mengi ya kijadi hasa kwa wanawake pamoja na binti yake. Hivyo tunaweza kusema kuwa utenzi huu haujasadifu ushujaa bali umekuwa na wahusika ambao ni binti yake anayeitwa Mwanahashimu, (ubeti .37), wanawake wengine (ubeti 94), Mungu ambaye anatajwa katika (ubeti. 5, 23, 36,72,73,82, 87 na 88) na mume (ubeti. 42, 47, 48).
Mianzo na miisho ya kifomula, mwandishi ameanza na sala au dua kama kawaida ya tendi za Kiswahili, katika sura ya kwanza (ubeti.4-7) anamwambia mwanaye aketi chini na Mungu wa rehema atasaidia katika kufanikisha jambo hilo. Mfano (ubeti.4) anasema;
Ukisa kutaqarabuBismillahi kutubuUmsalie HabibuNa sahabaze pamoya.Pia anamalizia kwa shukrani ya kumshukuru Mungu kwa kumfanikishia shughuli nzima ya utunzi wa kazi yake na kuufanya usomwe na watu wengi ili uje kuwa nyenzo ya maisha yao. Mfano (ubeti.101-102)101. Mola tutasahiliaKwa Baraka za NabiaNa masahaba pamoyaDini waliotetea102. Nahimidi kisaliaKwa Tume wetu nabiaAli zake na dhuriaItwenee sote pia.MAUDHUI.
UTENZI WA MWANAKUPONA unaonekana kujadili masuala ya itikadi ya kijinsia yaani yakukubali na kuheshimu ngazi za mamlaka kama zilivyo bila kuzivunja kwa kuwa ni amri ya Mungu. Hata hivyo mawazo yake yanaonekana kuwa yalitokana na vyanzo kadhaa kama vile, mafundisho ya dini ya kiislamu, yanatokana na mila na desturi za Waarabu zinazofuatwa na wenyeji wa pwani, mtazamo na ozoefu wa tabaka tawala la pwani. Mawazo yote haya yanaunganika na kutupa dhima kadhaa kama zifuatazo.
Dhima za utendi huuKatika uchambuzi wa kazi yoyote ya kifasihi tunaona kwamba huwa na dhima mbalimbali ambazo huweza kuwa za kijamii, kihistoria na kiutamaduni. Lakini dhima hizo kwa kiasi kikubwa hutegemea muktadha na wakati wa utunzi wake. Kwa mfano utenzi huu ulikuwa na dhima zake nyingi kwa wakati ule lakini kwa sasa hauwezi kuwa na dhima ileile kwa kiwango chote kama ilivyokuwa wakati ule.
Kijamii, inaonyesha kuwa Mwanakupona aliuandika utenzi huu kwa kuzingatia tabaka lake na jamii yake. Kwani alikuwa katika jamii ya tabaka la Kifalme na hivyo dhima zake zilionekana kumsaidia zaidi binti aliyopo katika uwanja huo sio zaidi ya hapo. Kwa mfano alijaribu kuzungumzia masuala ya kutojichanganya na watumwa wakati wa kazi (ubeti. 20), kuepuka wajinga wasiojichunga (ubeti.21), kuwa mwaminifu na mpenda haki,(ubeti.14) kujinyenyekeza mbele za wakubwa, (ubeti. 15) kuepuka uropokaji (ubeti.19) kumheshimu Mungu na mtumewe (ubeti .23), kumheshimu mume (ubeti .31), kuheshimu wazazi, kuwa na upendo kwa wote (ubeti61-64), kuwa mtiifu (ubeti.13), kushika dini. Pia baadhi ya dhima hizo zinaonekana kuwa mwongozo kwa watoto wa kike mpaka kwenye jamii ya leo hii, na labda ndio maana tunauona unafaa mpaka sasa. Pamoja na kugusia hayo hakujaribu kuzungumzia maswala ya tabaka la chini kama vile kulima, pamoja na maisha ya tabaka la chini kwa ujumla ila tu, anamwambia mwanaye awasaidie watu wasiojiweza mfano (ubeti.64) Anasema;Na ayapo muhitajiMama kwako simuhujiKwa uwezalo mbujiAgusa kumtendeaHapa anadhihirisha wazi kabisa kuwa yeye anatoka katika tabaka la juu na kila kitu anacho.Kihistoria, utenzi huu unatuonesha kuwa ni utenzi wa kale yaani wa miaka ya 1858 ambao ulitungwa na Mwanakupona kwa lengo la kumwonya binti yake na wanawake wengine. Ulikuwa na mashiko zaidi kwa wakati huo na kwa kiasi fulani mpaka sasa unaonekana kushika chati kwani unatoa maonyo na maadili kwa wanawake wa kisasa kama vile kuepuka umbeya, kuacha uvivu (ubeti .37), kuwa na adabu (ubeti.13), kushika dini, upendo kwa wote, wanawake kuwaheshimu waume zao pamoja waume kuwaheshimu wake zao.
Kiutamaduni pia utenzi huu unaoneka kuwa kwa kiasi kikubwa unazungumzia mambo ya kitamaduni hasa utamaduni wa kufuata mila, desturi na jadi za Waswahili, na kwa kiasi kidogo unagusia pia tamaduni za Kiarabu. Kwa upande wa Waafrika kama tunavyojua kuwa wao wana mila na desturi zao za kijadi ambazo hutokea baada ya kijana kuonekana anafikia hatua ya makuzi. Hivyo jamii huchukua jukumu la kuwafunda vijana wa kike na kiume. Kwa mfano hufundwa kuhusu mambo ya ndoa (namna ya kuishi na mume) na maisha kwa ujumla. Hata ndani ya utenzi huu tunaona hayo yakifanywa na mtunzi kwa binti yake, akimwonya juu ya mambo kadhaa ya kiutamaduni kama vile; adabu na heshima, kuepuka umbeya, kuepuka fitina, kuepuka uchoyo (ubeti.64), kuepuka uvivu (ubeti .37), kuwa msafi na kujipamba ili kufurahisha na kumvutia mume ubeti. (40-42), kutomnyima mume chochote anachokitaka (ubeti.29) na kumhudumia kitandani mfano. (ubeti.31) anasema.
Kilala siikukuseMwegeme umpapaseNa upepo asikoseMtu wa kumpepea.Funzo hili liko katika mila za ndoa kwani utamaduni wa Waswahili husisitiza sana masuala kama hayo hasa kwa kudumisha ndoa kwa kupendana na kutimiziana mahitaji mbalimbali ili kuishi kwa furaha na amani ndani ya nyumba mfano kutabasamu kwa mke kila anapomwona mume wake (ubeti.50).
Pia utamaduni wa Kiarabu ulioguswa ni kama vile; namna ya mwanamke anapovaa na kutoka nje ya nyumba yake inatakiwa aweje, mwandishi anatuonyesha kuwa Waarabu wanatamaduni zao ambazo wanazifuata na kuzitekeleza lakini kwa sasa zinaonekana kabisa kuingia katika utamduni wa waswahili na tunazifuata. Kwa mfano masuala ya kutawishwa kwa mwanamke pamoja na mavazi (ubeti 44-45), pia mwanamke anaambiwa kuwa anapotoka asiangalie wala kuongea na watu njiani, (ubeti .46) anasema
Wala sinene ndianiSifunue shiraaniMato angalia tiniNa uso utie haya.Tunaona kuwa hizi ni mila za kiarabu ambazo kwa sasa zinaonekana kuleta athari mpaka kwetu mpaka sasa.
Suala la dini, sehemu kubwa ya UTENZI WA MWANAKUPONA unaonekana kujadili zaidi kuhusu maudhui ya kidini na kusisitiza haja ya kuzingatia mafunzo ya dini ya kiislamu. Kama vile, kumtii Mungu na mtume wake (ubeti.23), kupenda na kutenda haki kama dini inavyotaka (ubeti. 12), kumtii mume na kuishi naye kwa upendo kama dini inavyotaka. (Ubeti.26-27), pia utenzi huu unatufundisha kuwa Mungu pekee ndiye anayeweza kutenda chochote unachohitaji na kama ni hivyo basi hatuna budi ya kutanguliza maombezi yetu kwake popote tunapofanya jambo fulani hata baada ya kumaliza shughuli yoyote ni vyema pia kumshukuru. Mfano huu tunauona pia kwa Mwanakupona mwenyewe ambaye alianza kwa dua na kumalizia tena na dua ubeti. (4-7, 66-102).
Falsafa ya mwandishi juu ya utenzi huu inaonekana kuwa mwanamke hawezi kufika mbinguni kama hajamtendea mume wake mambo anayopaswa kufanyiwa katika maisha ya ndoa.Hivyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa UTENZI WA MWANAKUPONA unaonekana kuwa nguzo ya mafunzo na maonyo kwa wanawake hata wa kizazi cha sasa lakini kwa kuangalia kwa baadhi ya mafunzo ambayo yanaendana na wakati huu maana mafunzo mengi yaliyoelezwa ni ya wakati wa zamani na hayana maana kwa wakati huu. Pia utenzi huu unaonekana kumdidimiza sana mwanamke hata kutopewa uhuru wa kuweza kufanya mambo mengine ya kimaendeleo kwani unamfanya mwanamke muda wote awaze namna ya kumriwaza mume tu.
MAREJEOMulokozi, M.M. (1999) Tenzi Tatu za Kale. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili: Dar es Salaam.Senkoro, F.E.M.K (2011) Fasihi. Dar es salaam. KAUTTU.
Uchambuzi wa makala ya mwandishi Jan Vansina. Hapo Zamani za kale: Mapokeo Simulizikama historia ya Afrika
MUHTASARI WA MAKALAMwandishi anaanza kwa kumnukuu Mbope Luis wa Kongo anayesema “ vitabu vyetu vipo kichwani mwetu”.
Makala imejaribu kuelezea historia ya masimulizi jadi yaliyokuwa yanapatikana Afrika. Mwandishi aanatofautisha jadi za namna mbili kwa kutumia jamii za Kiafrika na za Ulaya. Anasema kuwa tofauti na Ulaya ambako kusoma na kuandika vilikuwa kama kielelezo cha ustaarabu, jamii za Kiafrika kabla ya kuja ukoloni zilijitosheleza na kujieleza kwa kutumia mapokeo simulizi. Mwandishi anasisitiza kuwa nafasi na dhima ya mapokeo simulizi barani Afrika iliendelea kustawi hata baada ya kuingia kwa ustaarabu wa kusoma na kuandika, kwa maneno mengine Vansina anakiri kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya jadi ya mapokeo simulizi na jadi ya maandishi. Katika kulithibitisha hili anamtumia Profesa Willam A. Brown ambaye aliikuta barua huko masino ( Mali ) ambayo maudhui yake yalielezwa kwa kurejelea mambo mbalimbali. Yaliyokuwa yamesahaulika lakini yalikumbukwa kutokana na barua hiyo, barua hiyo ilikuwa kama chombo cha kutunza kumbukumbu hizo ili kurithisha desturi hizo.Muundo, mfumo na dhima ya mapokeo simulizi ya jamii hubadilika kutokana na maingiliano yanayotokea katika jamii ambayo husababishwa na mabadiliko ya kuachwa kwa vitu muhimu katika wakati maalum na hatua za mabadiliko hayo huitwa muundo wa usahaulifu “structural amnesia” kwa kuwa masimulizi jadi ya jamii, utamaduni ulirithishwa kwa mawasiliano ya ana kwa ana na kubadilisha maudhui, kila jamii ilieleza; imani, maadili, mawazo na mtazamo wake katika fasihi.
Levis Straus anazungumzia muundo ndani wa mazungumzo, anasema kila kinachozungumzwa kina muundo kama huo, ila hujidhihirisha zaidi katika masimulizi. Muundo huu unahusisha msukumo, mtiririko wa maonesho, kujenga kilele kimoja au zaidi, usambamba, uradidi na kubadilika kwa onesho na hivi vyote lazima vichanganuliwe kabla.
Pia anasema athari yake katika maudhui yanaweza kuonekana na mtu yeyote anayechanganua maana ya ishara “ taswira za tendi” au taswira maarufu katika historia.Katika nukuu ya Levis Straus na wanaantropolojia waliofuata walisema masimulizi mengi yalikuwa ya kitalii.
Kila tarihi ilieleza muundo halisi wa ishara za msingi zinazoeleza sio vitu vyenye thamani tu vilipendwa na jamii ya watu kiundani lakini pia utendaji wa kifikra wa binadamu, fikra za mwanadamu hazina budi kuwa na ushirikiano wa kifikra kabla ya kuelewa na kuwasiliana.
KUSUDI LA MWANDISHI
Kusudi la mwandishi katika kuandika makala hii ni kutaka kuthibitisha kuwa Afrika kulikuwa hakuna masimulizi, mfano ngano, tendi, misemo, hadithi (masimulizi).
NAMNA ALIVYOPANGA KUSHUGHULIKIAAlishughulikia suala hili kwa kupitia tafiti za wataalamu wengine ambao tayari walikuwa wameshafanya utafiti kuhusu mapokeo simulizi, mfano alimtumia Ernest Bernheim, ambaye katika utafiti wake alidondoa nyimbo, ngano, na saga, hekaya, masimulizi mafupi, misemo na methali.Pia alimtumia Profesa William A. Brown kwa kutumia barua yake ambayo aliikuta huko Masino ( Mali) iliyokuwa na maudhui mengi kuhusu Afrika.
Baada ya hapo aliamua kufanya tafiti yeye mwenyewe ili aweze kuziba pengo la wale wataalamu wengine na kuweza kulinganisha kile walichokipata wataalamu waliopita na kile alichokipata yeye kuhusu mapokeo simulizi ya Kiafrika.
JINSI ALIVYOPATA DATAAliangalia masimulizi ya Warundi na Warwanda na kuona kuwa masimulizi ya waburundi yalikuwa mafupi kwa sababu yanatolewa katika mkusanyiko usiokuwa rasmi lakini masimulizi ya Warwanda yalikuwa katika mchanganyiko yaani marefu na mafupi.Pia waliangalia nyaraka zilizoandikwa, makumbusho sanaa halisi, malighafi ya tamaduni na habari ya Wanaismu. Japokuwa data zote hizi isipokuwa ile ya matini iliyoandikwa na zilikuwa zimesomwa na wataalamu wengine.
Zilizoandikwa katika Afrika zilifanywa na wageni ambao hawakuelewa shughuli za jamii na tamaduni walizoshughulikia. Aligundua kuwa nyaraka za zamani zilikuwa na ukweli zaidi, mfano kwa kutumia barua aliyoikuta Masino ( Mali ) na kwa kuangalia masimulizi ya Warwanda na Waburundi.DATA HIZO ZILIKUWAJE?Jan Vansina anasema jamii nyingi za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara zilitumia mapokeo simulizi kwa muda mrefu, japokuwa zilitumia maandishi kwa kiasi kidogo, hivyo zilitawaliwa na jadi ya kimasimulizi. Kila kitu kilichohusu maisha yao, ikiwemo historia yao kilihifadhiwa katika masimulizi hayo. Hivyo mwanahistoria yeyote mwenye nia ya kutaka kuifahamu historia ya Wafrika hana budi kutambua kuwa mhimili mkuu wa historia ya jamii hiyo ni mapokeo simulizi.Kwa upande wa Tanzania maeneo mengi ya kati, mapokeo simulizi yalikuwa chanzo kikuu cha historian a maarifa mpaka miaka ya 1880, ambapo historia ya falme za Kongo zilikuwa zimebadilishwa kuwa katika maandishi.
Hayo mapokeo simulizi yalitumika katika siasa ya kijamii, kiuchumi, dini, misafara mbalimbali na shughuli za kiutamaduni.Data hizo pia zilionyesha mwingiliano wa matini katika mapokeo simulizi, kuhusu hili Vansina anasema suala la mwingiliano matini huhusisha ujitokezaji wa vipengele vya nyimbo za kidini, methali, ngano, katika mapokeo simulizi kama masimulizi ya kijadi yaliwekwa katika mpangilio ( tarihi za matukio mbalimbali ).Kwa upande mwingine Vansina anafafanua kuwa nyimbo maarufu katika baadhi ya jamii ziliimbwa kwa kurudiwa mara nyingi na zingine kwa nadra. Kwa mfano katika familia za kifalme miongoni mwa jamii za Bushoong ya Kasai (Kongo) nyimbo hizo ziliimbwa kipindi cha kumsimika mfalme. Huko Afrika Magharibi miongoni mwa jamii ya Wadogoni nyimbo hizo ziliimbwa katika shughuli za kidini na kijamii kama vile matambiko na sherehe za kijadi. Katika jamii hii, nyimbo mashuhuri zilizohusu matambiko na sherehe za kijadi zilisimuliwa kwa jamii nzima hasa mara moja kila baada ya miaka sita.HITIMISHO LAKEKutokana na utafiti wake alioufanya kwa kutumia data mbalimbali, alihitimisha kwa kusema kuwa Afrika kuna jadi ambazo zimetokana na masimulizi.UFAWAFU WA MAKALAKila jamii ina umuhimu wake hata kama inatimiza kwa kiasi kidogo mambo mazuri au malengo au dhima yake inaweza kubadilika kipindi cha urithishwaji kwa sababu jamii imebadilika, tathmini ya kuharibika ambayo hutokana na msukumo katika jamii wakati mwingine ni vigumu kukadiria.Kuna uhusiano mkubwa kati ya mapokeo simulizi na maandishi, katika kuthibitisha hili anamtumia Profesa William A. Brown aliyeikuta barua Masino ( Mali ) ambayo maudhui yake yalielezwa kwa kurejelea mambo mbalimbali yaliyosababishwa lakini yalikumbukwa kutokana na barua hiyo.Jadi nyingi za Kiafrika ni za kimasimulizi zikifungamana na nyimbo na mashairi lakini haziangukii katika aina ya jadi za Ulaya. Pia kimuundo zipo kama masimulizi, ndefu kuliko zilivyo hadithi zingine.Maelezo hayo yana mchango mkubwa kwani yanadhihirisha kuwa Afrika kulikuwa na tendi ambazo zilikuwa katika umbo la masimulizi na kishairi.MAPENDEKEZOMwandishi alipokuwa akisema jadi zimetokana na masimulizi hususani ushairi. Je huo ushairi ulikuaje? (ushairi ulikuwa unafuata kanuni au lah!) kwa hiyo utafiti ufanyike zaidi ili kujua huu ushairi ulikuaje.Kama hizo jadi zilikuwa katika usimulizi, usimulizi huo ulikuwa ni rasmi au sio rasmi? Tunapendekeza mwandishi afafanue kuwa jadi zimetokana na usimulizi gani haswa, kwa hiyo tafiti ziendelee kufanyika.HOJA NZITO1. Uasili wa kijadi unaweza kuwa wa namna mbalimbali, kwanza kwa kushuhudia matukio, pia kutoka katika maandishi, mfano ngano ubunifu wa matukio ya kihistoria au shughuli za kifasihi, visa vya kubuni pamoja na vya kuiba.
2. Afrika kuna tendi ambazo zimetokana na masimulizi ya kijadi.3. kuna uhusiano mkubwa kati ya masimulizi jadi na maandishi.4. Nyaraka zilizoandikwa katika Afrika zilifanywa na wageni ambao hawakuelewa shughuli za jamii na tamaduni waliyoshughulikia.5. kila jadi ina umuhimu wake hata kama itatimiza kwa kiasi kidogo mambo mazuri au maadili.6. muingiliano matini katika masimulizi jadi ni jambo ambalo haliepukiki mfano; nyimbo za kidini, methali, ngano, yaliwekwa katika mpangilio (tarihi ) za matukio.HOJA TETEJadi za ulaya zina muundo rahisi lakini zina mpaka rasmi na ni za kawaida katika ubora.JAMBO MUHIMU KATIKA MAPOKEO SIMULIZI YA KIFRIKAMapokeo simulizi yamekuwa yakitumika na yanatumika zaidi na zaidi katika historia ya Afrika. Mtiririko huu ni ushahidi katika makala za kihistoria za Kiafrika. Tangu mwanzo mwa mwaka 1960 makala zilikuwa na angalau kipengele kimoja kwa mwaka kilichokuwa kikizungumzia mapokeo simulizi, katika vipindi vyote vitatu vya karibuni vya historia ya Afrika Mashariki vimekuwa vikielezea Mapokeo simulizi kati ya mwaka 1500-1850, hasa sehemu za kati ya Tanzania.
Utaratibu wa kukusanya mapokeo simulizi unapatikana kwa kufuata utaratibu wa kutafuta tamaduni za kifamilia au hata kwa kuona, kuhesabu matukioa kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Kwa mfano, katika kipindi cha ukoloni tukio kama vile vita vya majimaji (1905-1907) Afrika Mashariki. Hali kama hii pia ilipatikana huko Afrika ya kati na maeneo ya Sudan.Jitihada za kukusanya na kuhifadhi data za kimapokeo simulizi zinadhihirika pia huko Jamhuri ya Niger ambapo tunafahamishwa kuwa kuliandaliwa eneo maalumu kwa ukusanyaji na utunzaji wa sanaa jadiyya. Swali ambalo mwandishi anajiuliza ni kuwa pamoja na kuwepo kwa jitihada za kutosha katika kukusanya na kuhifadhi data za mapokeo simulizi hakuna haja ya kujiuliza maswali kuwa Mapokeo simuliz yanaweza kutumika kama chanzo cha taarifa za kihistoria?. Anaendeleza mjadala kwa kusema kuwa haja ya kujiuliza ipo kwani suala hili linategemea namna ya ukusanyaji na uchanganuzi wa data.
No comments:
Post a Comment