UBUNIFU


                                                       


N
YAYO ZAO ZIMEPOTEA.
NAIKUMBUKA SIKU AMBAYO NILIAMKA NAKUSIKIA SAUTI YA MAMA NA BABA WAKISEMEZANA CHUMBANU KWAO. KATIKA MAZUNGUMZO YAO NILISIKIA MAMA AKIONGEA KWA KUTOA SAUTI YA KULIALIA KIDOGO KAMA ANAYEUMIA HIVI! WAKATI BABA NAYE SAUTI YAKE HAIKUA NZURI ZAIDI, SI UNAJUA MKE NA MME!! AU HAUJAWAHI KUSIKIA HIZO SAUTI ZA CHUMBANI!!! BASI NGOJA NIKUSIMULIE JINSI SAUTI HIYO ILIVYO KWANI KATIKA MAONGEZI YAO NILISIKIA MANENO MAWILI ALIYOSEMA MAMA WAKATI NIMEBANA SIKIO LANGU VIZURI KATIKA MLANGO WA CHUMBA CHAO,  SIKIO LANGU HALIKUTAKA KUBANDUKA, NILISIKIA MAMA AKIMWAMBIA BABA “MME WANGU NYAYO ZETU ZIMEPOTEA”HAY!! MOYO WANGU ULIENDA MBIO, NILINYANYUA MGUU WAGU KUANGALIA KAMA ZA KWANGU ZILIKUWEPO, HA! HA! HA1 HA! KUMBE HAKUMAANISHA HIVYO YEYE ALIMAANISHA HIVI Ni kweli wakoloni walitutawala na kutuachia sumu kali iliyotufanya tuwe hivi kama tulivyo. Katika sababu zilizotumiwa na wakoloni wakati wanakuja katika nchi za kiafrika walisema wanakuja kutustaarabisha. Ni kweli kwani kipindi hicho hatukuwa na uwezo wakukataa kwani tuliwaona wazungu kama watu wenye mwonekano wa pekee kuliko sisi. Tuliwatukuza na kuwaheshimu kwachote walichofanya nakutufundisha. Mfano “assimilation policy” tulikubali kwani hatukujua madhara yake.
Baada ya wakoloni kuondoka tulibaki wenyewe tukijidai kuwa tunajiongoza, nikweli tunajiongoza kwani si hatuoni mzungu amkiwa amekaa ikulu! Hivyo moja kwa moja najua kuwa tunajitawala. Mengine usiniulize kwani naandika kulingana naninavyojua na kuona mfumo ulivyo. Yote tisa kumi ni kuhusu ustaarabu tulioletewa na wazungu.
Nakili kuwa kabla yaujio wa wazungu wazazi wetu walikuwa wamestaarabika zaidi. Hii nadhani kila mmoja ananiunga mkono, kwani nikitu gani mababu zetu walikuwa hawana na kipi walikuwa hawatimizi! Nadiliki kusema kuwa wazee wetu walikuwa na akili nyingi ila zilikuja kuharibi wa nawakoloni. Lakini pamoja nahayo wazee wetu hawakuharibika moja kwa moja kiasi kwamba wakashindwa kujitambua, kijijua na kuelewa sehemu waliyopo pamoja na utu wao.
Sasa wakoloni walishaondoka miaka mingi tu, wazazi wamezaa watoto na watoto wamezaa na mpaka kufikia leo hii. Lakini wazazi wasasa wamekiuka mila na desturi zawazazi wao waliowazaa na kusababisha kizazi wanachotengeneza kuonekana kama cha kiwenda wazimu. Siwezi kukulaumu moja kwa moja wewe kijana mwenzangu wa kike na kiume kutokana na mambo unayofanya. Mzigo huu nautua kwa wazazi wanaokulea, hivi kupindi cha wao kuzaliwa mbona masuala haya hayakuwepo? Na yanakuja kuonekana leo? Hivi wewe mama unapoamua kutembea kifua wazi ukionesha mashina ya maziwa yako unamaana gani?? Hivi mimi mwanao najifunza nini kutoka kwako? Mama unaamua kuweka kifua chako njembele ya mwanao tena wa kiume!! Duh! Usisemee cheni na misalaba yaYesu inayoonekana imepasua katikati ya maziwa. Mamaaaaaa! Hiyo misalaba mnaidharirisha!
Jamani! Mungu alimuumba mwanadamu akaziweka sehemu zinazopaswa kuonekana wazi na zile zisizopaswa kuonekana wazi, pia ukizingatia na utamaduni wa mwafrika, hivi kweli mama unapopita mbele ya mwanao akiwa amekaa na baba yake unajihisi vyema kweli! Au? Sumu hii imeenea kwa wanenu, pita njiani kote angalia watoto wa kike na kiume wamepotoka kabisa, hawajui wafanye nini, hawajui nguo ya kuvaa kulingana na mukutadha, sasahivi nguo ya kuogelea inavaliwa ofisini, nguo ya ufukweni inavaliwa sebuleni, nguo ya usiku inavaliwa mchana yaani hakuna anayejari. Mungu wangu! Yote haya wanarithi kutoka kwa wazazi hasa kina mama.
Wapopia kina baba wasiojari mwonekano na maadili ya wanao, lakini kwa kiasi wanajaribu kukemea ila wadada wanapewa vichwa na mama zao. Samahani kwakuwagusa moja kwa moja. Mtoto wa kike anarejea ndani na nguo hiyo ya ajabu, mama umekaa huulizi eh! Unafurahi kumuona mwanao anaonesha mapaja yake, kitovu pamoja na maziwa yake yaliyostahili kufichwa hadi siku yanaonwa na mme wake, lakini leo hii kila mtu anayaangalia, hivi utakuwa najipya gani mbele ya mumeo??????????? Huangalii maadili gani mwanao anaelekea, unaona yote sawa tu eee! Unamharibu huyo, kwanza anajipunguzia thamani kwa kila anyemuangalia, anapewa sifa mbaya mara kahaba, muuaji, kibaka, kweli! Majina haya yanamfaa kulingana na mwonekano wake. Ndiyo.
Pili kutokana na kuonesha viungo vyenu vya siri mnapunguza uthamani wake, mnaanza kuonekana kama vitu vya kawaida ambavyo ukienda sokoni au barabarani unaviona. Sehemu iliyolindwa na ya thamani sana, leo hii naiona wazi duh! Mnapoteza hamu watoto wa kike jamani. Hebu mjirudi siyo kila unachoiga ni kizuri kukiweka katika matendo, najua Mungu kajaria mnamiliki simu kubwa za viwango, kwenye mitandao huko ndo mnashinda TV ndani usiseme. Unatumia muda wote kuangalia ni nguo gani kava mwanadada wa Ulaya ili nawe uvae uonekane kama, yeye! unapotea yeye anasababu ya kuvaa vile. Natabiri japo mimi si mtoto wala sina undugu na familia ya marehemu ShekheYahya ila kufikia mwaka 2015 kina dada watatembea uchi LIVE na akina kaka vilevile hapo ndo tutakuwa tumekamilisha safari yetu ya kurudi kipindi cha ujima.
WAKATI AKINA DADA WANAKAZANIA KUPANDISHA SKETI ZAO KUTOKA MAGOTINI KUPANDA JUU, KINA KAKA WANAKAZANA KUSHUSHA SURUALI ZAO KUTOKA KIUNONI HADI MAPAJANI. SIJUI NI MASHINDANO AU?
BABU ZETU WALIKUWA NA MAADILI WALIOTULITHISHA SASA TUNAYAMALIZA, WAO WALIVAA MAGOME YA MITI LAKINI NDIYO ULIKUWA UTAMADUNI WAO NA HAWAKUWAHI KUSEMA WANA AIBU KUVAA VILE, SASA USTAARABU WA LEO UKO WAPI? KATIKA KUVUA NA KUTEMBEA UCHI! AU TUNARUDI TENA KATIKA KIPINDI CHA UJIMA NINI!!!, LABDA “EVOLUTION” INAANZA TENA. ILA KIUKWELI INAUMA.HASA KWA WAZAZI KUONEKANA NDIO MSTARI WA MBLELE BADALA YA KUONYA NA KUTOA MISINGI ILE WALIYOFUNDISHWA NA WAZAZI WAO.ZIKO WAPI NYAYO WALIZOPITIA BABU ZETU ZA MAADILI???? NDIO ZIMEISHAPOTEA, KWELI ZITAREJEA????????????
JIBU LA YOTE UKIULIZA UTAAMBIWA NI “UTANDAWAZI KAKA! TEMBEA UONE MAMBO YA KALE TUMEACHANA NAYO, TUNAFANYA YA KISASA BABA. HAAYA ILA……………….


 USIDHARAU USICHOJUA.
Haikuwa rahisi kwa kila mmoja kuamini maneno yangu niliyotoa huku machozi ya uchungu na furaha yakilowanisha nguo niliyotoka nayo huko baada ya kushinda adhabu kali, nilijiona tajiri mkubwa na tangu siku hiyo niliamini kuwa utajiri si mpaka uwe na majumba na pesa. Hebu fuatisha kisa hiki ustaajabu yaliyostaajabiwa na majaliwa katika ……………..
Kila siku iendayo kwa Mungu Majaliwa aliongozana na baba yake kwenda kutega mitego ya wanyama mwituni. Mzee huyo aliitwa Byansheko aliyekaa katika kijiji cha Katuruka. Mzee huyo alifurahia sana hasa alipokamata wanyama kama swala, chui, simba, nyati na wengine wengi walioleta manufaa katika familia yake. Mzee huyo alitumia ngozi ya simba na chui katika biashara haramu ndiyo maana alifurahi sana alipoua aina hiyo ya wanyama. Kila siku mzee huyo  na kijana wake waliweza kutega mitego zaidi ya kumi na mara nyingine mitego yote  ilinasa wanyama au siku nyingine alikosa kabisa.
              Siku  moja alitega na kukuta  mitego yote imeteguka lakini ikiwa haina kitu chochote. Mzee huyo alijawa na furaha akiwa bado mbali alipoona miti yote aliyotumia kutega imesimama wima alijua tayari amekamata viumbe kumbe wapi mitego ilikuwa imesimama tu pengine huteguliwa na upepo uliouvuma au nyani ambao walirukia na kukaa juu ya mti uliopindwa na mitego hiyo huteguka na nyani hao huvamia na kula vile vyakula alivyoweka ili awakamate. Katika taratibu zake za kutega na mwanae, mwanae alianza kujua kupinda mti na kuweza kutega mitego kwa umaahiri . Kwa kuwa baadaye alijua kutega basi mara baada ya baba yake kuishiwa nguvu aliona bora amwachie mwanae kwani damu yake ilikuwa bado inachemka. Hivyo alimwachia kazi hiyo na kuamua kustaafu. Alivyoacha mwanae ndiye alichukua nafasi na kuanza kwenda mwituni peke yake.
Kadri siku zilivyozikuenda ndivyo Majaliwa alivyozidi kunawiri kutega na kukamata wanyama; mara nyingine alitega mara mbili kwa siku, siku  moja alicha ametega mitego mitatu tu aliporudi jioni yake alikuta mitego yote ina wanyama, majariwa alifurahi sana, lakini akiwa bado anafurahi alifika kijana mmoja jina lake Mswadiko. Kijana huyo naye alikuwa mtegaji hodari lakini alikuwa akitega katika eneo tofauti na lile aliliokuwa akikitega Majaliwa.
Siku moja Majaliwa alipokuwa anarudi kuangalia mitego yake, alikuta mtego mmoja umemnasa  faru. Kwa kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kumnasa mnyama huyo Majaliwa alimkimbilia kama alivyokuwa amezoea. Kabla hajamfikia mnyama huyu alionesha uchungu aliokuwa nao kwani mtego ulikuwa umembana sana. Mnyama huyo alifoka kwa hasira alipomuona kijana huyo akimkaribia. Majariwa alimkimbilia kama kawaida yake ambavyo  aliwakimbilia wanyama wengine. Baada ya kumfikia Faru huyo alinyanyuka pale alipokuwa na kumvamia  Majaliwa na kumpiga pembe lake mguu wake wa kushoto . Majaliwa alitoa sauti ya kuumia sana japokuwa hakuwepo mtu aliyemsikia ambaye angeweza kumsaidia alitua mbali kidogo na mtego faru huyo aliyezidi kufoka akimwangalia Majaliwa pale alipokuwepo.  Faru huyo alionesha hasira, alijivuta sana kwenye mtego ule ili amfikie na kummaliza lakini kulingana na ufupi wa kamba ile na uimara wa mtego faru huyo hakuweza kumfikia Majaliwa.
Majaliwa aliendelea kugalagala pale chini bila  kupata msaada, aliunguzwa na jua, kwani hakuweza kujikokota kutoka eneo lile. Baada ya muda mrefu kupita alikuja mwenzake kuanagalia kile ambacho Majaliwa alipata siku hiyo. Baada ya kufika eneo lile alishangaa kuona Majaliwa hajamtoa mnyama yule katika mtego wake, pia alishangaa kwani alikuwa haoni dalili yoyote ya kuwepo kwa mtu mazingira yale. Aliangaza huku na kule baada ya  kitambo kupita alidhani kuwa huenda Majaliwa alikuwa ameondoka na kuacha ametega mtego huo labda faru huyo kakamatwa mchana huo.
 Lakini chakushangaza ni kuwa hata siku moja hakuwahi kuona wanyama hasa maeneo yale wakitembea muda wa mchana sasa itakuwaje mnyama huyo akamatwe na mtego mchana huo? Kijana huyo alinyemelea taratibu kuuelekea mtego ule, kichwani aliwaza kuwa kama angekuta rafiki yake hayupo basi angenufaika na kitoweo hicho. Baada ya mawazo hayo kijana huyo alikaribia mtego ule lakini alipotupa kando macho yake alikuta  Majaliwa akiwa hoi taabani  alimsogelea kumsaidia lakini huku akiumia kupoteza bahati ya kupoteza kitoweo hicho.
Kijana huyo alimnyanyua Majaliwa na kumweka kivulini. Alipomwangalia alishangazwa na donda kubwa lililokuwa katika sehemu ya paja ya mguu wakushoto Majaliwa. Kijana huyo alimsaidia wakokotana hadi kufika nyumbani kwao na mara baada ya kufika Majaliwa alimwekea dawa ya asili iliyoaminika kuwa ilikuwa na uwezo wa kutibu majeraha haraka sana. Kwa muda wa miezi mitatu majariwa na mwenzake hawakuweza kurudi tena mawindoni. Kijana yule kwa kuwa alionesha sana moyo wa kumtembelea na kumsaidia rafiki yake Majaliwa siku moja aliulizwa na wazazi wa Majaliwa kuwa anaitwa nani? Alijibu “Simoni”. Kijana  alionesha moyo wa huruma kwa mwenzake na kumhudumia kila siku.
Kwa kuwa watoto hao hawakubahatika kwenda shule, shughuli yao kubwa ilikuwa ya kuchunga na hasa shughuli yao kubwa sana ilikuwa uwindaji. Baada ya muda mrefu wa kuuguzwa majeraha baba yake Majaliwa alimwambia “Mwanangu sikia kwa kuwa kazi hii ya uwindaji imekufanya kilema kwani sasa huwezi kutembea kama siku zile, basi naona ungeachana nayo tu kwani sasa inaonekana badala ya kutoa faida tumetoa hasara” Majaliwa alikubali kwani aliyekuwa anaongea alikuwa mzazi wake na asingeweza kupuuzia ushauri wake.
Simoni aliendelea na shughulika na uwindaji na hakukata tama kwani ndiyo ilikuwa shughuli iliyomwingizia kipato mara baada ya kuuza nyama. Baada ya kugundua kuwa kuna wanyama hatari aliwekea tahadhari kubwa sana kwa wanyama alifikilia yasije kumkuta yaliyomkuta mwenzake. Haikupita muda mwingi mzee Byansheko alifariki kutokana na kuugua sana. Hii ilikuwa nafasi nzuri kwa Majaliwa kuendelea na kazi yake ya uwindaji. Vijana hao walivamia tena pori na kujendelea kutega mitego yao.
Siku moja Majariwa alitega mitego yake kama kawaida lakini hakupata kitu chochote, siku ya pili hivyohivyo na wiki ikapita bila kupata kitoweo chochote lakini mwenzake alipata kila siku. Baada ya kuongea na rafiki yake alimwambia kuwa huko mawindoni alikutana mtu wa ajabu., mtu huyo alikuwa na mguu mmoja na alitembea kwa kurukaruka. Alisema kuwa mtu huyo alipendezwa sana na mitego ya Simoni lakini akamwambia  angependa kila siku aendelee kupata kitoweo basi kila anapotega mtego aimbe wimbo huu,

                                      Akogaya niko kabutosa, akogaya niko kabutosa
                                    Liba nategile lugayo mulye. Leba nategile lugayo mulye
                                 Amagezi gawe galakulokola, amani gawe tigakulokole
                              Anapiga makofi mara tatu mara baada ya kuimba wimbo huo

Alivyozidi kuimba wimbo huu ndivyo alizidi kupata vitoweo vingi. Aliona akimfundisha na mwenzake basi wote wangekuwa wanapata kitoweo wote. Baada ya Majaliwa kuambiwa wimbo huo alipotega mitego yake aliimba wimbo huo tena kwa sauti ili kila mnyama ndani ya mwitu asikie na kujongea eneo lile. Baada ya kwenda kushuhudia mitego yake kama kawaida yake alikuwa akiangalia kwa mbali kabla hajafika aliona mitego yote minne imesimama     alifurahi sana kwani alijua siku hiyo alikuwa amejipatia kitoweo cha kutosha.
Baada ya kuifikia mitego yake hakuamini alichokuta alipigwa na butwaa na kubaki akiwa amekodoa tu macho. Amlimfikiria vibaya rafiki yake aliyemfundisha wimbo ule usiokuwa na maana yoyote. Katika mtego wa kwanza alikuta umenasa buibui, mtego wa pili ulinasa radi, mtego wa tatu ulinasa ndege na mtego wa mwisho ulinasa mdudu aina ya nzi. Majaliwa hakufikiria kuwatoa lakini baada ya muda vyote  kwa pamoja vilitoa sauti ya kuomba msaada ili vitolewe kwenye mtego na kwamba siku moja vingemsaidia katika mazingira tofauti. Majaliwa aliona ajabu na kuogopa sana kuona radi, ndege nzi na buibui wanaongea!  Alikimbia kwenda kumuita rafiki yake na mara baada ya kufika sehemu ile walikuta bado vimenasa katika mtego.
Simoni alitumia busara na kumwambia mwenzake awatoe kwenye mitego kwani hii ni dunia na hatujui ni wapi tutaishia, hivyo pamoja na Majaliwa kuvitoa mitegoni  bado alikuwa amejawa na nafsi ya woga, akadhani yale yalikuwa mazingaombwe ya kichawi. Tangu siku hiyo Majaliwa aliachana na  uwindaji.
Alipofikia muda wa kuoa Majaliwa ilibidi atafute mke wa kuoa, katika pitapita alimpata binti mzuri aliyesifika katika eneo lile. Binti huyo aliwahi kuchumbiwa na watu wengi sana matajiri lakini binti huyo aliwajibu kuwa wa kwake hajazaliwa. Pamoja na kuwa wasichana wengi waliolewa kwa kuangalia maslahi lakini binti yule hakuweza kujali maslahi. Alimtaka mtu ambaye atampenda na kumlidhiia mwenyewe bila kuwepo kwa msukumo wa mtu yeyote. Kwani alishaona wengi waliolewa na wenye mali na kukosa upendo wa mtu na kukaza upendo katika mali tu. Hivyo binti huyo alikataa jambo hilo japo familia yake nayo ilikuwa ya kifalme; Kijana Majaliwa pamoja na umaski wake hakusita  kumwambia dada huyo kuwa anampenda sana na kuwa angeona vyema kuishi naye katika maisha yake yote.
Alimwuliza “Samahani dada unaitwa nani?” Akamujibu. “Maria” “Maria, Maria, Maria umeolewa?” Naye akamwuliza na wewe mwenzangu  waitwa nani? Kabla ya kukujibu kama nimeolewa au la! Naitwa “Majaliwa. Maongezi yaliendelea katika maongezi ya Maria alijaribu kupeleza maisha ya Majaliwa kwani yote waliyoogea alijitahidi kumuuliza maswala kuhusu maisha yake na familia yake na kugundua kuwa alikuwa mtu wa nasaba ya chini sana.
Aligungua kuwa Majariwa alikuwa anatoka katika familia ya kimaskini iliyoishi kwa kutegemea nguvu ya uwindaji. Pia Majariwa alionekana kuwa kijana dhaifu asiyeweza kufanya jambo lolote kutokana na familia alimotoka. Katika maongezi na dada huyo, dada alionekana kuvutiwa na maisha ya Majaliwa pamoja na kumsimulia kuwa alitoka katika familia maskini. Maria alifikiria kati ya wachumba waliomjia hakuweza kumpata mwanaume wa nasaba ya chini ambaye alifikiria kuwa ndiye angeweza kuyalinda maisha yake kwa kumwekea tunu ya upendo kuliko wenye mali wanavyoweka moyo wote katika mali na kusahau wenzi wao.
 Majaliwa hakuamini macho yake baada ya kuona mtoto wa familia ya kifalme kukubali kuchumbiwa na kuolewa na mtoto wa mwindaji maskini kama na yeye. Aliona kama kiteendawili kwani hakuwahi kufikiria kuwa maskini anaweza kuoa kwa tajiri, na hakuwahi kushudia jambo kama hilo. Maria alimtolea wasiwasi na kumwambia kuwa hata wazazi wake wakimwekea vikwazo hatakuwa tiyali kuwakubalia kwani mapenzi ya kweli ni yamtu kujichagulia amtakaye. Maria alifikiria hivyo kwani haikuwa desturi kwa mtu maskini kuoa katika familia yao.
 Taarifa ilifika kwa wazazi wa Maria na ilipokelewa kwa shingo upande hawakujua kuwa Maria angekubali kuchumbiwa na kijana kama yule na walijua kuwa mwanao angekataa katakata kuolewa na maskini. Asiye kusaidia kubeba hajui uzito wa mzigo, binti Mariamu alikuwa ameishatua mzigo wa moyo wake kwa kijana fukara Majariwa. Baada ya kuhojiwa  binti yao kuhusu kijana huyo aliwajibu kuwa huyo ndiye mvulana wa maisha yake aliyemsubilia kwa kipindi kirefu.
Wazazi walipigwa na butwaa kuona binti yao anang’ang’ania  kuolewa kwa kijana yule. Hivi  Maria umerogwa! Yaani badala ya kuongeza akili yako kwenda mbele unataka kuirudisha nyuma kwa kuolewa na fukara huyu! Baba aliwamaka kwa hasira. “Bora kuolewa na fukara atakaye nijali kwa upendo kuliko kuolewa na tajiri anayewazia mali muda wote kuliko upendo” Maria alijibu.
Baada ya kuona hivyo kuwa binti yao ameishaamua waliamua kuweka mikakati kabambe  kuhakikisha kijana huyo anashindwa kumuoa binti huyo. Kijana huyo alipewa mitihani migumu ambayo kiuhalisi asingeweza kuishinda. Mtihani wa kwanza aliopewa alioneshwa miamba mikubwa akpewa nyundo mpya na kuambiwa apasue miamba hiyo ndani ya dakika kumi na tano na kupewa sharti kuwa nyundo hiyo haikupaswa kuwa na alama yoyote ya kupinda.
 Kijana huyo kabla hata ya mtihani wa pili alihisi tayari amesindwa kwani isingewezekana kupasua miamba hiyo kwa nyundo na nyundo hiyo isiwe na alama yoyote. Akiwa bado anatafakari namna ya kupasua miamba ile gafla ulisika mgurumo mkali kama kwamba kuna dariri ya mvua, ilitokea radi na kumwambia “Nakumbuka we ni rafiki yangu”, Rafiki yako! Rafiki yako yupi? Majaliwa aliuliza kwa hofu, we ni rafiki yangu uliyeninasua katika mtego na nikakuahidi kuwa siku moja nitakusaidia sasa naona leo ndiyo siku yangu ya kukusaidia naona umepewa mtihani nzito usioweza kuutatua bila msaada wangu” radi ilimwambia. Hivyo nakuomba usogee mbali kidogo na ufumbe macho nifanye kazi yangu.
 Majaliwa alisogea pembeni na kufumba macho ulitokea mlipuko kubwa wa radi na kupasua miamba hiyo ikiwa kama kokoto, lakini mlipuko huo aliusikia Majaliwa tu. Na baada ya kufungua macho alikuta mawe yote yakuwa kokoto.
Majaliwa alienda kutoa taarifa kwa wazazi wa binti na wazazi hao hawakuamini walichokiona baada ya kukuta miamba ikiwa kokoto na nyundo ikiwa kama alivyokuwa. Ilibidi wabadilishe zoezi na wakaona kwa vyovyote vile kijana yule angeshinda na kumuoa binti yao kipenzi aliyekataa kuolewa na tajiri wakati wazazi wake ndicho walichopenda.
Hivyo walipanga pigo jingine la kumkomoa kijana huyo asiweze kumuoa binti yao. Walimwaga gunio ala ulezi katika mchanga na kumwamulu aokote ulezi huo bila hata kuchanganya na mchanga na alipewa dakika chache tu. Baada ya kufanya hivyo walijua hata kwa siku tano asingeweza kumaliza kuokota ulezi huo. Hivyo waliondoka na kumuacha akihangaika  kuokota punje mojamoja na kuweka katika gunia lake.
 Haukupita muda walifurika ndege wengi wadowadogo na kuanza kumsaidia kwani ya yeye aliwahi kuwategua katika mtego wake. Muda haukupita mwingi gunia hili lilijaa na ndege hao waliondoka haraka sana kabla ya wazazi wa Maria kuingia. Haikupita hata nusu dakika tangu ndege hao watoke wazazi wa Maria walingia. Walikuta Majaliwa kasha maliza ila anajaribu kupekua tena katka mchanga ili kuona kama angeona punje nyingine iliyobaki alimladi asije kunyimwa mke. Lakini pamoja na kupepesa macho yake hakuona hata chembe ya ulezi hata moja iliyokuwa imebakia. Wazazi hao walizidi kutahamaki na kuanza kumhoji kitugani kinamsaidia kufanya maajabu kama yale.
Baada ya kuona kijana huyo anakuwa tishio waliamua kumkomoa kwani, kwani pesa kitu gani isichofanya waliamua kuhama duniani walimoishi na kuhamia mbinguni ambako walijua kuwa kijana Majariwa asingeweza kufika na angekata tamaa na kuacha kumfuatilia binti mfalme huyo. Baada ya kuwa wamefika mbinguni,  binti  yao alionekana kuchukizwa sana na maamuzi ya baba yake kwani alijua ndiyo  anampoteza mpenzi wake.
  Taarifa ilitolewa kwa kijana yule kuwa kama anataka kumuoa binti wa Mfalme basi amfuate mbinguni. Kwa mawazo ya kijana yule alijua kuwa labda binti huyo atakuwa tiali amefariki na hivyo ilikuwa tu taarifa ya kumjulisha kuwa bora atafute binti mwingine. Pia aliwaza namna ya kuweza kufika huko. Alikatatamaa na kujua kuwa bora tu abadilishe mawazo ya yule binti na kutafuta binti mwingine kwani kisicho riziki hakiliki.
 Akiwa anawazia hivyo alionekana buibui akining’inia kutoka mbinguni kuelekea alipokuwa  amesimama Majaliwa na kumwambia “rafiki yangu usiwaze sana nipo kwa ajii yako hivyopunguza fikra  lazima ushinde mitihani yote na lazima umuoe binti huyo na huku nitokako nimemuacha hai ila analia kila saa akiwaza kukupoteza lakini hatakupoteza.” Majaliwa alishtuka kuona hadi buibui huyo anavyojua siri ya kuwa Majaliwa anamfuta binti mfalme. Muda sumuda bibui aliweka tandu lake na kumwambia Majaliwa apande, safari ya kuelekea mbinguni ilianza.
 Lakini wakati huo Majaliwa alimiwa afunge macho yake ili asije akaogopa maana mbinguni ni mbali. Majaliwa alifananya hivyo na baada ya muda alijikuta amesimama mbinguni.  Baada ya kuingia alikutana na walinzi ambao walikuwa wanalinda lango kuu la kuingia kwa mfalme. Baada ya kujieleza walinzi hao walikubali kumsaidia na kumpeleka kule alikowaambia.  Kufika kule wazazi wa Maria walipata taarifa lakini hawakuamini kama ni kweli kwa waliyoambiwa lakini waligundua kuwa ni ukweli pale walipoonana kijana waliyemkimbia uso kwa uso. Walizidi kushangaa kuona kila mtihani unaotolewa kijana huyo anaufaulu.
Baada ya siku tatu wazazi wa Maria waliona wamrusu akaolewe na yule ampendaye lakini akipata matatizo asiwalaumu wazazi kwani walisha mweleza yote kuhusu watu maskini wasio na mwelekeo. Lakini mama yake Maria hakuwa tiali kumluhusu mwanae aolewe hivihivi bali aliona bora waweke hata mtego mwingine ili akiushinda basi atakuwa amefanikiwa kumuoa mwanao kipenzi Maria. “Utaweka kipingamizi kipi kingine, kama ameweza kutufuata hadi huku mbinguni itakuwaje ashindwe kutatua mtego wako unaotaka kumuwekea” alijibu baba “sikia huyu kijana kwanini asiuawe? Mbona kawa king’ang’anizi au? Kama mnaona haiwezekani semeni, lakini mimi siko tayari mwanangu niliyejizalia kuolewa na hohehahe”. Alimaka mama. Ulipopangwa mtego wa kuangamiza sehemu aliyokuwa anakaa Majaliwa, lakini pindi wana panga hayo yote Maria aliyasikia yote  yaliyopangwa. Aliamka usiku wa manane na kuelekea kwa mpenzi wake Majaliwa na kumweleza yote yaliyopangwa, alimwabia kuwa siku inayofuata asilale ndani kwani kibanda chake kinge chomwa moto. Siku iliyofuata kibanda cha Majaliwa kilichomwa moto na yeye hakuwemo ndani ya kibanda hicho bali alijificha mbali kidogo na kibanda chake na kushuhudia yote yalikuwa yanatendeka.
Asubuhi yake familia ya Mariamu ilikuwa ikifurahi kuangamiza kijana huyo asiyekuwa na hatia alichotaka ni kuoa binti wa mfalme. Wakiwa katika furaha hiyo alitokea Maria na kusimama mbele ya wazazi wake japo katika tamaduni mwanamke hakutakiwa kuvuka mlango wa sebule na kuja sehemu ya akina baba lakini yeye alifanya hivyo. Alikaa kama dakika mbili bila kusema kitu huku ameinamisha kichwa, wazazi wake walidhani kuwa anamlilia Yule kikaragosi aliyepigwa kiberiti na kuangamia.
Maria aliinua kichwa na kusema “wazazi wangu nimevunja mila hii na kuja kusimama mbele yenu wakati haikuruhusiwa, naomba mnisikilize, mimi ni mtoto wenu mliyenizaa na kunitunza hadi leo hii nikuwa mkubwa, sijawahi kufanya dhambi yoyote mbele yenu wazazi wangu, mlivyonizaa ndivyo nilivyo sijawahi kukutana na mwanaume yoyote maishani mwangu, nilisubilia mwanaume ambaye ningemchagua mwenyewe na mwanaume niliyemchagua mimi ni Majaliwa ambaye ninyi wazazi wangu hamuhitaji.
 Baba na mama na nyinyi ndugu zangu mambo ya kuchaguliwa wanaume ni hatari kwani mnaye mchagulia huwa hana upendo kama yule anayejichagulia, naomba mniruhusu niolewe na mwanaume wa chaguo langu, Majariwa” Majaliwa yupi? Marehemu eh au kuna Majaliwa mwingine? Mama aliuliza kwa kejeri “mama sikia kitendo mlichonya cha kwenda kumuua Majaliwa hamkumuua” eh! “taarifa yote mliyopanga ninimwambia , hivyo mliunguza kibanda tu wakati yeye akiwa amewaangalia hivyo yupo na hakufa” wazazi walitahamaki na kumfuza binti yao mbele yao.
Baada ya kuona hivyo wazazi hawakuwa na jinsi nyingine waliamua kumuita kijana huyo na kumpa mashrti ya siku ya kuja kumuoa binti yao. Masharti hayo ni kwamba watapangwa wasichana kumi na watapakwa matope mwili mzima na kupangwa katika msitari mmoja na Majaliwa alitakiwa kumgusa mara moja tu aliyempigania yaani Maria. Na angeshindwa basi angekuwakuwa amejipotezea bahati. Siku ya kumchagu mke wake Majaliwa ilifika lakini kijana huyu alitetemeka sana kwani alifikiria namna ya kuweza kumchagua  mtu aliyepakwa tope mwili mzima tena wakiwa kumi, akiwa anawaza alikuja nzi akamnong’oneza Majariwa “yule nitakaye mwendea naomba umchague yuleyule ujkichgua tofaujti utakuwa umepoteza bahati. Majaliwa hakibisha alifanya kama alivyoambiwa na mara alipoitwa kuchagua mchumba wake ni yupi majaliwa alifuatia pale yule nzi alipogota na kumtoa huyo msichana katika msitari.
Baada ya kumuangalia alikuta ni binti mfalme mwana wa tajiri aliwekewa vikwazo vingi kuolewa sasa anaolewa na kijana wa chaguo lake aliyemlilia siku nyigi. Wazazi wa Maria hawakuwa na jambo la kufanya tofauti na kuwatakia maisha mema na yenye mafanikio katika familia mpya iliyoenda kufunguliwa na vijana wawili waliopendana na kuvumiliana na kusaidiana. Wapenzi hao waliishi maisha safi ya fuhaha. Wote walisimuliana maisha waliyopitia na Majliwa alimsimulia mke wake kuhusu mitego ya ajabu ya radi, nzi, buibui,na ndege kuwa ndio wamefanikisha hadi wanaoana. Pia alimsimulia na mitihani yote aliyopewa na wazazi wa Maria katika harakati za uchumba. Walicheka wote kicheko cha furaha wakakumbatiana na kubusiana kwa ishara ya upendo. Tangu siku hiyo Majariwa na mkewe huheshimu kila kitu katika dunia hii.

                                                       RAHA YA KUWA MSHAIRI

 
NI WEWE TU
Umeiteka akili yangu, sina pakuegemea
Watawala mawazo yangu, sina cha kukuambia,
Wanipangia chakufanya, sina cha kujivunia,
Kisa  niliyekuchagua, maisha yangu kuyaangalia.

2. Akili haijitambui  usemalo nazingatia,
Sina haki kukuuliza naogopa kuumizwa
Nazifuata zako sheria yangu hayana nyongeza
Upeo wangu wa mbali, sasa wana karibu.

3. maneno yako yalinivutia, ukalimu wako ulikuuza,
Kwa upendo uliniahidi maisha mazuri kunipatia,
Sasa  siku zapita sioni lolote linlotokea,
Najutia upendo niliokuonesha, nakumbuka niliyemtosa.

4. sherehe nyingi unaandaa, sioni ukinialika,
Jamani huoni haya! Kwa mali zangu unazotumia!
Wapambe, marafiki wajivunia jasho langu
Niliye wa ndani naishia kuangalia.

5. Sherehe zikimalizika, wadai fuko limepungua,
Magoti waludi kunipigia, wataka na kilichobakia
Waenda pia kwa wa jomba na makaka usiowajua,
Upendo wako kwangu waupoteza, matumaini nimepoteza.

6nafasi yako nitaheshimu ikiwa, ikiwa utaniheshimu,
Ulinikuta na maisha ya kati, sasa niko maskini
Sina cha kujivunia, upendo wako tiari umeniangamiza,
Ila nasubili mapinduzi.

NAJIVUNIA KISWAHILI
1. Lugha yangu yapendeka, najionea fahari,
Najitangaza kwa umma, ulimwengu ujue,
Najivunia, najitabia lugha  yangu ya Kiswahili.

2. Siwzi saliti lugha yangu, kama wakubwa zangu,
Ofisini wajigeuza wazungu, kiingeleza kwa kuiswahili,
Tuiludieni fahali yetu, twapendeka kwa lugha yetu.

3. wananchi wanyimwa uhondo, kiingereza kikitumika bungeni,
Kiingereza mwajua ninyi, watanzania wengi waswahili,
Kiingereza tunakariri, jukwaani twajiaibibisha.

4. wageni wamiminika, vyuoni kujifunza,
Mfano hai tosha, cha pendeka,
Kwanini unapapatika, lugha yako kuipoteza?

5. nawasihi watanzania, wasomi hasa mkinisikia,
Tuache kuipondea, lugha yetu imetulea
Kwa kiingereza tunapotea, hasara tunajitia.

6 mfano huu nawatolea, kila mmoja afikiri,
Mazao mengi yanapotea, lugha ya madawa hawaijuia
Kiingereza yameandikwa

7. yote nayaongea, moyoni naumia
Kiswahili nasomea, vyovyote nitapigani,
Umma magoti nawapigia, utamaduni wa Kiswahili kurudia.


 
UMEPOTEA
We dada umepotea,wapi unaelekea?
Huko unako kimbilia, hebu rudi utaangamia.
Jamii iankuangalia, ulimwengu unakulilia.

2 utamaduni wako ukowapi, mbali umetupia!
Dada na kaka nawuliza, maswali yangu mnayasikia?
Matendo mnayofanya shule gani mnatoa?

3 nguo fupi mnavalia, hiyo ni njia ya kupotea,
Usitazame wavaliao hivyo, tazama utu wako,
Heshima wajipotezea, nzi wadudu wanyama wakuchekelea.

4. mungu alikutumba kwa mfanowe vitabuni twaambiwa,
Uzuri wake kakupatia, ngozi nzuri kakauwekea,
Waona alikosea wataka kumkosoa!

5vipodozi unavyotumia, kiama wajiandalia,
Magonjwa yakunyemelea, kansa mkono imekutegea
Madawa unayotumia, fikiria wanaotengeneza wanatumia?

6 hili moja najiuliza, wazazi wanayaona?
Wengine wasaidia  wanao kujiharibia
Mila mbaya mwawafundisha, eti kizazi kipya!.

7wazazi wetu wamkua, vliitu vya asiri walitumia,
Uzuri hawakulazimisha, walitumia mola alowajalia,
Nawe nakusisitiza, uzuri haulazimishwi,
Ukifanya hivyo jua njia uokovu umeipotea.

 

HII NDIYO SIMU?
Simu kifaa cha mawasiliano, chaisaidia jamii,
Haraka ujumbe utafikisha, bila muda kupoteza,
Wasifika sana ewe simu, kwa kusema unayoambiwa.

2 lakini simu mezua jambo, simu waongea uongo,
Familiaa meongeza migogoro, ndoa nyingi umevunja,
Koo umetenganisha, simu gani waleta balaa?.

3 ukiwa ofisini wajibu uko nyumbani, wakwepa deni kulipa,
Simu waongeza umaskini, dora kila siku kukununulia,
Huangalii nani wala nani, ukiisha zira ujumbe hutompelekea.

4 mpenzi wangu simuamini, mpaka nimuone machoni,
Hata ajibu yuko kazini, nitaamini kwa kuuliza jirani,
Simu watutia mashaka jamani, mioyo yetu tena haina amani.

5 nauliza yupimsaliti, simu au mpiga simu,
Awe ndugu yangu usiiamini simu.

 

LA AZIZI.
Sioni haya wal yale,moyo wangu umeushika,
Meachia moyo wangu utawale, kiumbe uliyetukuka,
Mwenye umbo la kipare, hisia zangu umezishika,
Akili yangu waipa misele, kichwani yanirukaruka.

3. una sura nzuri na tabia ya kuvutia
Hupendi makuzi, hasa kwa usiye mjua,
Hujitii kiburi kujifanya wajua,
Kwa mazuri jibu huwezi kukawia,
Hata kama yana dosari, jibu utafikiria.

2.umbo lenye mvuto, kama mhaya na ndizi,
Na maneno yako ya mkato, yananinyima usingizi,
Nitafanya mchakato, kujifunza zote pozi,
Ili uingie kwenye mpakato  unitibu na zako pozi.

4.macho ya mviringo, na kichaka cha nywele,
Wayazungusha bigobigo, ntakuacha unitawale,
Waonekana mbongo, kumbe mtoto wa kipare,
watazama kwa maringo, mithili ya ndege kware.

5.kifua nyongo kiuno, siyo unafiki umepewa,
Binti usiye na majivuno, ukitembea wajiachia,
Mwana usiye na matukano, mema pekee wapendelea.
Miguu na yako mikono, uzuri yakuongezea,
Neno gani nikwambie nahisi nitaboa
                                            
                                             6. wapenda kujisifia, si kwa uzuri wala tabia,
Ila kwa uliyemtunukia, moyo wako kukumbatia,
Wanifanya niweze kujisikia, pale pote ninapokuwa,
Najiona shujaa, kwa imani uliyonijengea,
Najua ahadi wanitunzia, ya pendo tulilioahidiana.

7. ulimwengu umeamini, heshima yako kali,
Usiyependa vimini, mara nyingi suluali,
Nani asikuthamini, wakati wajithamini
Dharau  waweka mbali, tulia ujae mwangu moyoni.

8. sijamaliza zote sifazo kuzitoa,
Za ndani nakuachia, moyoni nimezipakia,
                                              moyo wangu nimefungua, nafsi yako nakutunzia,
Mikono miwili nakutegea, sala nyingi najiombea,
Kwa wazazi bukoba kukupeleka, ndizi senene kukupatia.


 
KWA NINI?
1.Aa! Baba, aa! Mama,
Kwa nini?
2.kipenga kilipolia cha uwanjani mliingia,
Mchezo mliufaulu golini mkaniweka,
Kazi yenu kunilinda nisije porimoka.

3.Goli ni latumbo, mtoto anamokaa
Hiyo ndiyo nyumba yake mola alomjengea,
Ulinzi mkubwa kamwekea jeraha lolote kutompata.

3. ndani ya nyumba mnamwangamiza kemikali mkitumia,
Pombe sigara mkitumia maisha yake mwampunguzia,
Azaliwa kabla ya wakati, kwanini?

4.imani potofu mtajitia mwanenu kalogwa,
Mmemloga wenyewe kwa sumu mlompatia,
Ni kwa raha zako mama maisha yake hukuangalia.
Kwa nini?
5. kweli ulipenda raha sasa imekuwa karaha
Ndiyo amezaliwa kilema raha itaendelea?
Fikiri kabla ya kutenda.







UTAKE USITAKE. upepo
Kuanzia mwanzo nadondoa, macho yangu yalichokiona
Mtaani nimepitia, wakazi wengi nimeona,
Shughuli ndogo wajifanyia, kipato kidogo kujipatia,
Maisha ya dar ninavyoyajua adabu wengi yanawati.

2vibandabanda wanjenga, njini na kando ya barabara,
Masoko horela waibua, mji kutoutambua,
Stendi ya ubungo ukipitia, mfano mzuri utajionea,
Kinachowasukuma ni maisha, hakuna anayejitakia.

3kasheshe huingia, safisha mji ikaribia,
Utakeusitake utaondoka, popote we elekea
Ukibisha utasurubika viboko utakavyo patiwa,
Mabanda yote huoezwa, mali zote husambalatishwa.

4 machinga mama n’ntilie aendewapi, kijiwe hicho amezoea
Nyanya na malighafi zake ndani zinamuozea,
Shule watoto na mke, machinga wamwangalia,
Ee waende waapi jamani mbona nchi imewachukia?

5 ewe unayenipiga mateke, tazama ulikotokea,
Kazi uliyonayo nami naweza kuwa nayo,
Mkubwa anyekutuma naye namwambia,
Mabavu hayatawali busara ndiyo mwongozo.

6vibaka mtani mwasema wanaongezeka,
Wakianzisha miradi mara moja mwaipoteza,
utamalizaje mgogoro kwa kuanzisha mgogoro?



DAR ES SALAAM.
Dar es salaam jiji zuri watanzania twajisifia,
Kwambali yaonekana, kwenye ndege ukiwa umekaa,
Nalisifia jiji la matajiri, na makabwela waliozagaa,
Wenye mwingi uchovu na mioyo ilyo kata tama.

2 jiji lenye umati wawatu, mchana hadi mchana,
Waonekana kama siafu, karikoo Buguruni pitia,
Usijiulize wanalala wapi, kukicha njiani kawaida unawaona,
Kila mmoja atafuta riziki kutimiza yake mahitaji. 

3   jiji lenye watu wenye kubadilika bila kujari wakati,
Watu wasiojari uwepo wa wengine,
Leo eneo laonekamna safi kipitajioni utashika pua,
Jamani jiji la watu mbona linakuwa takataka kila sehemu?

4   jiji lenye waswahili wengi,wenye wingi utapeli,
Machoni waonekana wema, ati watu wasafi,
Wasiopenda kufanya kazi, vijiwe vya kahawa waamkia,
Wajiita wasafi kazi hawataki fanya, jioni wakabaji

No comments:

Post a Comment