Fasili
ya taaluma ya fonolojia haiwezi kukamilika, na pengine kueleweka iwapo hakuna linalosemwa
kuhusuiana na taaluma ya fonetiki. Hali hii inatokana na ukweli kuwa kuna uhusiano
wa kinasaba kati ya fonolojia na fonetiki. Massamba na wenzake (2004:5)
wanaeleza ukweli huu kwamba:
Fonetiki
na fonolojia ni matawi mawili tofauti ya isimu lakini yenye kuhusiana sana.
Uhusiano wa matawi haya unatokana na ukweli kwamba yote mawiliyanajihusisha na uchunguzi
na uchambuzi unaohusu sauti za lugha za binadamu.
Kutokana
na ukweli huu, jitihada za kufasili dhana ya fonolojia inaelekea kuwa nyepesi,
dhana hizi mbili zinapofasiliwa kwa mlinganyo. Tuanze na fonetiki.
Fonetikini Nini?
Fonetiki
ni tawi la isimu linalochunguza sauti za kutamkwa na binadamu ambazo huweza kutumika
katika lugha asilia. Massamba na wenzake (kama hapo juu) wanafasili fonetiki kuwa
ni tawi la isimu linalohusika na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu za utoaji,
utamkaji, usafirishaji, usikilizaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa
ujumla. Wanasisitiza kwamba, kinachochunguzwa katika fonetiki ni (maumbo mbalimbali
ya sauti zinazoweza kutolewa na alasauti za binadamu (yaani sauti za binadamu zinazotamkwa
tu). Kipashio cha msingi cha uchambuzi wa kifonetiki ni foni.
Foni
ni sauti yoyote inayotamkwa na binadamu na inayoweza kutumika katika lugha fulani.
Hivyo basi, foni ni nyingi sana na hazina maana yoyote. Wanafonetiki hudai kuwa
foni zimo katika bohari la sauti
(dhana dhahania) ambalo kila lugha huchota sauti chache tu ambazo hutumika katika
lugha mahususi. Sauti chache zinazoteuliwa na lugha mahususi kutoka katika bohari
la sauti huitwa fonimu.
Matawi
ya Fonetiki: Kuna mitazamo miwili tofauti kuhusiana na matawi ya fonetiki.
Mtazamo wa kwanza ni ule unaodai kuwepo matawi
matatu; na mtazamo wa pili ni ule niunaodai kuwepo matawi manne. Mtazamo wa kuwepo
matawi matatu unataja fonetiki matamshi, fonetiki akustika, nafonetiki masikizi.
Mtazamo wa kuwepo matawi manne. (kama Massamba na wenzake ( kama hapo juu),
pamoja na matawi tuliyokwisha yataja, wanaongeza tawi fonetiki tibamatamshi.
Fonetiki
mahuchunguza jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti. Hususani,
huchunguza namna na mahali pa kutamkia sauti husika. Fonetiki akustika
huchunguza jinsi mawimbi ya sauti yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha
mtamkaji hadi kufika katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi hujihusisha
na mchakato wa ufasili wa sauti za lugha, hususani uhusiano uliopo baina ya
neva za sikio na za ubongo. Na fonetiki tibamatamshi ni tawi jipya lililozuka
mwanzoni mwa karne hii, ambalo huchunguza matatizo ya utamkaji ambayo binadamu
huweza kuzaliwa nayo au kuyapata baada ya kuzaliwa. Ni tawi linalojaribu
kutumia mbinu za kitabibu kuchunguza matatizo na namna ya kuyatatua.
Fonolojia ni Nini?
Fonolojia
ni taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya sauti za kutamkwa zinazotumika katika
lugha asilia mahususi za binadamu. Inapolinganishwa na fonetiki, inasisitizwa kuwa
fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza mifumo ya sauti za lugha mahususi tu, kama vile sauti za kiswahili,
Kiingereza, Kikongo, n.k. Hata hivyo, wapo wanaisimu wanaoelekea kukubaliana kuwa
kuna fonetiki ya lugha mahususi pia, na kuna fonolojia ya jumla, na fonetiki ya
lugha mahususi. Mathalani, Massamba (1996) licha ya kufasili kuwa fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mfumo wa sauti
za lugha mahususi, anaenda mbele zaidi na kudai kuwa fonolojia inaweza kuchunguza
sauti kwa ujumla wake bila kuzihusisha na lugha mahususi.
Akmajian
na wenzake (2001), nao wanadokeza msimamo kama wa massamba wanapodai kwamba
fonolojia inaweza kuchunguzwa kwa mitazamo miwili tofauti. kwanza, fonolojia
kama tawi dogo la isimu linalochunguza mfumo na ruwaza za sauti za lugh
mahususi ya binadamu; pili fonolojia kama sehemu ya nadharia ya jumla ya lugha
ya binadamu inayohusika na tabia za jumla za mfumo wa sauti za lugha asili za
binadamu. Katika mhadhara huu, hata hivyo tutakuwa wafuasi wa mtazamo unaoona
kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mfumo wa sauti za lugha
mahususi, hivyo tuna kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya
Kiingereza, fonolojia ya Kiha, fonolojia ya Kihehe, na fonolojia ya Kibena.
Kipashio cha msingi cha fonolojia ni fonimu.
Fonimu.
Ni
kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno. Hivyo
basi, fonimu ina maana, kwa kuwa inaweza kubadili maana ya neno inapobadilishwa
nafasi katika neno husika. Foni chache zilizoteuliwa kutoka katika bohari la
sauti ili zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahususi ndiyo fonimu. Hivyo,
fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya fonimu za lugha hutofautiana kati
ya lugha moja na nyingine. Mathalani, Kiarabu kina fonimu ishirini na nane
(28), Kiswahili kina fonimu thelathini (30), Kifaransa kina fonimu thelathini na
tatu (33) na Kiingereza kina fonimu arobaini na nne (44). Sauti ambayo huweza kubadilishwa
nafasi yake katika neno lakini maana ikabaki ileile huitwa alofoni.
Alofoni
ni kishio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo fonimu moja hutamkwa na kuandikwa
tofautitofauti bila kubadili maana ya neno. Mfano:
·
Fedha na feza
·
Sasa na thatha
·
Heri na kheri
Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti
ya fonimu [sauti] moja.
Mitazamo
juu ya Dhana ya Fonimu.
Juhudi za kufasili
dhana ya fonimu zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali zimezua mitazamo
mbalimbali ya namna ya kuchambua dhana hii. Hadi sasa, mitazamo mitatu ifuatayo
ndiyo hujulikana zaidi.
(i)
Fonimu
ni tukio la Kisaikolojia.
Huu
ni mtazamo uliokuzwa na kutetewa na wanasarufi geuzi-zalishi, mwanzilishi wake
akiwa ni Noam Chomsky. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni dhana iliyo katika
akili ya mzungumzaji wa lugha. Mtazamo huu unadai kuwa kila mzungumzaji wa
lugha ana maarifa bubu ya idadi na jinsi ya kutamka fonimu za lugha yake
Chomsky anayaita maarifa haya kuwa ni umilisi (competence). Anadai kuwa maarifa
haya ya fonimu hufanana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wazungumzaji wa lugha moja
husika. Kinachotofautiana ni jinsi ya kudhihirisha (kutamka) fonimu hizo, yaani
utendi (performance). Chomsky anabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuhitilafiana
baina ya umilisi na utendi kutokana na matatizo mbalimbali ambayo mzungumzaji hukabiliana
nayo. Matatizo hayo ni kama vile uchovu, ulemavu wa viungo vya matamshi
(alasauti za lugha), athari za mazingira, ulevi na maradhi. Hivyo kutoka na hali
hii, fonimu hubaki kuwa tukio la kiakili, yaani kisaikolojia tu.
(ii)
Fonetikinitukio
la Kifonetiki.
Wafuasi
wa mtazamo huu wanaongozwa na Daniel James. Ambaye anaiona fonimu kuwa ni
{umbo} halisi linalojibainisha kwa sifa zake bainifu. Anadai kuwa fonimu
huwakilisha umbo halisi la kifonetiki na inapotokea kukawa na fungu la sauti katika
fonimu moja, sauti hizo huwa na sifa muhimu za kifonetiki zinazofanana. Hivyo,
fonimu ya Kiswahili ni kitita cha sauti za msingi pamoja na alofoni zake.
(iii)
Fonimu
ni Fonolojia.
Huu
ni mtazamo wa kidhanifu, ambapo huaminika kuwa fonimu ni kipashio cha kimfumo,
yaani fonimu huwa na maana pale tuinapokuwa katika mfumo mahususi. Mwanzilishi wa
mtazamo huu ni Nikolai Trubetzkoy. Yeye huamini kuwa fonimu ni dhana ya kiuamilifu
na uamilifu huu hujitokeza tu fonimu husika inapokuwa katika mfumo wa sauti wa lugha
husika. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni kipashio kinachobainisha maana ya neno.
Mtazamo huu hutumia jozi sahihi kudhihirisha dai lake. Mathalani, maneno baba
na bata yana maana tofauti kwa sababu ya tofauti ya fonimu /b/ na /t/. Mtazamo huu
hujulikana kuwa ni wa kifonolojia. Na kwa hakika, mawazo haya ndiyo yaliyoshika
mzizi zaidi katika taaluma ya fonolojia na ndiyo inayofunzwa hivi sasa katika sehemu
nyingi ulimwenguni.
UhusianokatiyaFonetikinaFonolojia
FONETIKI
|
FONOLOJIA
|
HuchungasautizakutamkwanaBinadamu
|
HuchunguzasautizakutamkwanaBinadamu
|
Ni
pana {huchunguzasautinyingi}
|
Ni
finyu {huchunguzasautichachetu}
|
Ni
kongwe.
|
Ni
changa.
|
Huchunguzasautipekepeke
|
Huchunguzasautikatikamfumo.
|
Huchunguzasautikwaujumla
|
Huchunguzasautizalughamahususi,
kama Kiswahili, naKinyeramba.
|
Kipashio
cha msinginifoni
|
Kipashio
cha msinginifonimu.
|
UhusianokatiyaFoninaFonimu.
FONI
|
FONIMU
|
Hazimamaana
|
Zinamaana
|
Zipopekepeke
|
Zimokatikamfumo
|
Nyingi
|
Chache
|
|
Huwezakujitokezakamaalofoni
|
Zinaponukuliwa,
alamayamabano, “{ }” hutumika
|
Zinaponukuliwa,
alamayamabanomshazari, “/ /” hutumika
|
kaka vipi? napenda kuandika makala ya kiswahili kuhusu umuhimu wa fasihi katika maisha ya kila siku. je nifanyaje??
ReplyDeletejambo la msingi kwanza fanya utafiti kuhusu kile unachotaka kuandikia, kinaweza kuwa kimekugusa wewe moja kwa moja au mwenzako ali mladi uwe na uwezo wa kupangilia mawazo na mwisho utafanikiwawazo hongera kwa kuwa na moyo wa KUKIPENDA KISWAHILI KWANI NDIYO LUGHA MAMA KWETU.
Deletekaka mi naomba unisaidie utata unaojitokeza wakati wa uandikaji irabu za kifonetiki
ReplyDeleteutata upo wapi yani kwa sababu unaposema irabu za kifonetiki ni zile ambazo hazihusiani na lugha yoyote ile na nafikiri zipo 20
ReplyDeleteasante kwa kuitukuza lugha yetu ya kiswahili.....................!!
ReplyDeleteJe nisaidie kuelewa iwapo ujuzi wa fonetiki ni muhimu katika usomi wa kiswahili
ReplyDeleteMimi naomba hoja tano za mfanano na uhusiano kati ya fonetiki na fonolojia.
ReplyDeleteNaomba kujua uhusiano baina ya fonetiki na fonolojia🔰
ReplyDeleteUtata kwa uhusiano baina ya fonolojia na fonetiki....vile umeeleza pale juu ni utofauti au ubusiano? Naomba kujua
ReplyDeleteKazi nzuri Sana nimeipenda
ReplyDeleteKazi nzuri isipokuwa hujaambatanisha marejeo
ReplyDeleteMerkur & Ferencia: Merkur & Ferencia Merkur
ReplyDeleteMerkur & Ferencia merkur - Merkur & Ferencia Merkur in Solingen, febcasino Germany - Merkur - 1xbet 먹튀 Merkur https://febcasino.com/review/merit-casino/ Merkur - MERKUR - Merkur & Ferencia Merkur apr casino